Home » Posts filed under lifestyles
Showing posts with label lifestyles. Show all posts
Showing posts with label lifestyles. Show all posts
Facebook kuja na mtandao mpya ‘Facebook at Work’
Facebook inaanzisha mtandao wa kijamii kwaajili ya wafanyakazi kuwasiliana na kushirikiana kuhusiana na masuala ya kazi.
Facebook at Work utaonekana vile vile kama Facebook ya kawaida, lakini watumiaji watakuwa na uwezo wa kutengenesha akaunti zao binafsi.Watumiaji watakuwa na uwezo wa kuchat na wenzao, kutengeneza mtandao wa kazi na kushare nyaraka mbalimbali.
Mtandao huo ambao tayari unatumika kwenye ofisi za Facebook, utakuwa mpinzani kwa huduma zingine kama Google Drive, Microsoft Office na LinkedIn.
UNATAKA KUFANIKIWA? HAKUNA NJIA YA MKATO KATIKA MAFANIKIO
Je huu ni ukweli kwamba hakuna njia ya mkato kuelekea
mafanikio? Inawezekana unasema ‘Awali hujui mambo yanayoendelea na utabakia
hivyo hivyo’. Kuna kitu nimeendelea kujifunza kwa watu matajiri wanaochipukia
kwenye Forbes magazine na kwingineko.
Siku chache zilizopita katika Kongamano fulani ambako
Mjasiriamali wa Kenya Julian Kyula na Heshan De Silva waliongea kutokana na
uzoefu na historia ya Maisha yao. Kitu kimoja cha kufanana ni kutumia kile
ulichonacho na uweze kukiendeleza kufikia kule unakotaka.
Hakuna Njia ya Mkato kwenye Mafanikio; Kama kuna kitu
ambacho hatutaweza kuendelea ni kupitia njia za mkato. Njia za mkato haziwezi
kujenga maendeleo yako wala hutoweza kuacha kitu kiuchumi. Kwanini? Kuwa na
fedha ambayo huna maelezo nayo au haujaiwekeza kwenye njia sahihi ni kupoteza
hiyo mali.
Mimi huangalia zaidi upande chanya zaidi kuliko upande hasi,
kwa kila mtu ambaye namtolea mfano naangalia upande chanya, kama una kitu hasi
juu ya yeyote huo sio upande wangu wa makala hii.
Kuna njia nyingi za utafutaji wa mafanikio “kama kupanda na
kuvuna” kitu ambacho watu wengi wanapenda, vilevile biashara za njia ya
mitandao ili upate kamisheni kwaajili ya watu wanaojiunga chini yako. Hizo
hazijawahi kuwa njia sahihi za kufanikiwa mara nyingi zinaishia kutapeliwa.
Kufanya kazi kwa umakini na sio kwa nguvu. Umakini
unaozungumziwa hapa ni kuwa na watu sahihi au mtandao sahihi wa watu kuhusu
biashara au bidhaa unayoifanya. Umakini huo utakusaidia kufikia malengo yako,
haimaanishi kwamba hautakutana na vikwazo mbalimbali ila je una umakini gani
kupambana na vikwazo hivyo?
Inabidi Ukuze kitu ulichonacho. Watu wengi tunaogopa
kuchukua hatua ya kuamini kwamba kitu ulichonacho kinaweza kuwa kitu kikubwa
cha kuweza kukutengenezea ajira yako na watu wengine. Tunakuwa na sababu nyingi
na za kutosha kuonyesha kwamba haiwezekani. Ila ukweli uko hivi kwako
haiwezekani ila kuna mtu sehemu fulani usiyoijua wewe kimewezekana. Hivyo
inategemea mtazamo wako ukoje. Vitu vingi tunavyovifanya sasa hivi wazee wetu
hawajawahi kufikiri kwamba vitawezekana lakini vinafanyika na wanaona vinawezekana,
hivyo badilisha unavyofikiri unaweza ukabadiisha matokeo ya vitu unavyofanya
kila siku. Nuia Kukua kimtizamo na kiutendaji.
KWANINI HUKUITWA BAADA YA USAILI? YAJUE MAKOSA YANAYOFANYWA KWENYE USAILI
Kama huna mtu unayemfahamu kwenye taasisi au kampuni
uliyoomba kazi, ni vigumu kujua kwanini hujaitwa baada ya usaili. Hivyo kuna
baadhi ya mambo ambayo yatakufanya usiitwe, na haya ni mojawapo;
1 1. Makosa katika CV
yako
Hiki ndicho kitu cha kwanza kwenye
orodha ya mambo yanayowaangusha wengi. Wakati unaandiaka CV yako au barua ya
kuomba kazi hakikisha tena na tena kama ulichoandika ni sahihi na hakuna makosa
ndani yake. Vile vile unaweza kumpa mtu mwingine aiangalie kabla hujaituma, ili
kukusaidia kuangalia makosa ambayo labda wewe hujaweza kuyaona. Hakuna mwajiri
ambaye anataka kuchukua jukumu la kurekebisha makosa uliyofanya wakati wa
kuandika.
2. Kutokuwa na ujuzi mzuri wa Usaili
Katika usaili wowote, kama ni ana kwa ana au kwenye simu
kujua kuongea lugha vizuri na matamshi yake ni jambo la muhimu sana.Lugha za
mtaani na vifupisho vya maneno vinawezekana katika maisha ya kawaida na
inakubalika kwa jamii ya watu wanaokuzunguka lakini hayaleti picha nzuri kwa
mwajiri hasa unapoyatumia kwenye Usaili. Hakikisa siku ya kwenda kwenye Usaili
, ulale vizuri na kama ni mtu wa kwenda kwenye starehe siku hiyo upunguze kwani
mtu ni rahisi kukugundua kama ulichelewa kulala.
2. 3.
Jumbe zisizoeleweka kwenye mitandao ya Jamii
Hili ni jambo la kizamani, lakini
lisikushangaze. Uwe makini kwenye mitandao ya jamii wewe unaweka vitu gani,
jumbe gani. Kama wakati wote unaonesha picha za wewe ukistarehe, kunywa pombe
na tabia zingine za ajabu ajabu unapoomba kazi zafisha anuani zako za mitandao
ya kijamii kabla ya kuomba kazi.
4. Kutokuonekana kwenye Mtandao
Hii haimaanishi ni kigezo cha kila kazi, ni baadhi ya kazi
tu. Ila kama unatafuta kazi kwenye Masoko, Uhusiano na jamii, Matangazo
,burudani na Nyanja zingize za habari waajiri wengi wanapenda kuona mtu ambaye
ana taswira nzuri na yenye nguvu kwenye mitandao. Kama haujui kitu gani
kinaendelea kwenye teknolojia ya habari tafsiri yake ni kwamba uko nyuma sana
katika kujua mambo yanavyotakiwa kwenda.
5. Kuwa mfuatiliaji Sana
Watu wengi hufikiri kwamba waajiri wanafanya kazi ya
kuwatafutia wao kazi. Ukweli ni kwamba taasisi zote za kuajiri zinataka kujaza
nafasi za kazi zilizowazi kwa wateja wao. Na wanashughulikia wateja wengi kwa
wakati mmoja na kujaza nafasi nyingi kwa wakati mmoja. Kwahiyo kumtumia mwajiri
email au kumpigia simu yule amabye hakukujibu usifikirie kuwa utaonekana kwamba
unastahiki ya kazi, ila watakuona unawachosha hivyo hawatahitaji kushughulika
na wewe.
6. Wewe si Mvumilivu Sana
Kwa upande mwingine, kuna waajiri wengine watakupigia kupata
habari zaidi kuhusu wewe, hakikisha unajibu kwa haraka na ufasaha wakati wote
unapopigiwa simu. Kama kila wakati mwajiri anakupigia na kukufuatilia sana
kuhusu habari zako inamaanisha hujamshawishi vyakutosha kwa kazi ile uliyoomba
na vinginevyo inaweza kuwa sahihi.
7. Umekuwa Ukijilinda ili watu wasiwasiliane na wewe.
Kila mwajiri anakutana na jambo hili. Mtu anaweka tangazo la
kutafuta kazi kwenye tovuti na anasahau kwamba litakuwepo hata baada ya kupata
kazi. Kama hujawahi kuwa na anwani kwenye linkedin au mtandao mwingine
usifikiri ni rahisi mtu kuwasiliana na wewe kuhusu kazi. Hata kama hupendi kazi
iliyotangazwa, usiondoe anwani yako au CVhuwezi jua kwamba utapata fulsa
nyingine.
8. Huna vigezo vya kupata kazi hiyo
Wakati umekata tamaa unafanya maamuzi ya kukatisha tamaa.
Hata kama huna kazi na huna hela ya kutosha , hivyo unaomba kazi sehemu nyingi
hata kama vigezo vyako havikubaliki haitakusaidia na hutapata nafasi ya
kuajiriwa. Kama kitu ambacho mwajiri atakujua kwa sababu mbaya ni wewe siku
zote kutokuwa na vigezo vya kazi.
Unapotafuta kazi hasa kwa makampuni yanayoajiri inabidi uwe
mkweli, nenda na wakati na mwenye maelezo ya kutosha, kwakuwa mwajiri ni daraja
la wewe kutokuajiriwa au kufanikiwa kitaaluma.
NJIA ZA KUPUNGUZA UNENE WA MWILI WAKO
Wastani wa maisha ya mtanzania (na waafrika wengi) ni miaka 40-50. Kati ya sababu kuu zinazopunguza uhai ni kuwa na afya mbovu, m akala ya leo in ahusu tatizo la unene wa mwili. Tatizo hili la u nene na uzito uliozidi s ababu yake kuu ni kutokujua namna ya kutunza mwili wako kwa kula vizuri na kufanya mazoezi. Unene usio wa kawaida ni tatizo kubwa kwa watu wengi hivyo kama wewe ni mmoja wapo na unataka kupunguza mwili wako, hizi hapa ni njia za kukusaidia kupunguza unene na kuwa mtu mwenye muonekana mzuri na afya njema. 1. Kula vizuri. Ipo mifumo miwili ya kula vizuri. Kwanza ni chakula unachokula na pili ni namna unavyokila chakula hicho. Ulaji bora wa chakula. Kuna ulaji wa kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache. Tumbo lina m i suli ina y ofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unaparilia zaidi mafuta mwili na kusababisha kukaa kwa m afuta tumboni bi la kutumika ambapo baadae i tapelekea mtu kupata kitambi . PENDEKEZO: Asubuhi kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo unywe chai na vitu vingine kama mkate au maandazi.
Namna ya kula matunda na mboga za majani kwa mpangilio mzuri. Watu wengi h u k o sea kula matunda na mboga za majani kwa usahihi. Nasema hivyo kwa maana ya kwamba w engi hula matunda baada ya chakula, hii si namna nzuri ya kula kwasababu vimeng’enya chakula (enzymes) zilizopo tumboni hufanya kazi kwa namna tofauti. Enzymes hizi namna zinavyo nyambua na kumeng'enya matunda ni tofauti na namna zinavyomeng’enya vitu vigumu kama nyama au vyakula vingine jamii ya wanga hivyo matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine. Ni bora kula matunda dakika 10-20 kabla ya kula chakula kwasababu unapokula matunda baada ya kupata chakula hugeuzwa na kuwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya mfumo wa damu kupitia utumbo mdogo, wengu, moyo, ini nakadhalika.
Mseto wa vyakula ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (“acid”) na vile vinavyomung'unyuka haraka (“alkaline”) havitakiwi viliwe kwa pamoja. Mfano mzuri ni matunda. Matunda yenye uchachu kama machungwa, mananasi na maembe yanatakiwa yaliwe pamoja na yale laini zaidi kama ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk nayo yaliwe kivyake kwasababu mfumo wake wa kumeng'enywa ni tofauti. Vilevile nyama nyeupe (nyama za ndege na samaki) unashauriwa ziliwe tofauti na nyama nyekundu (nyama za ng’ombe, mbuzi, kondoo nk) ziliwe tofauti. Chakula bora kwa afya njema. Kula vyakula bora vyenye thamani kwa mwili wako, epuka vyakula vyenye sukari nyingi, mafuta mengi au chumvi nyingi badala yake zidisha kula mboga mboga zilipikwa kiasi bila kuiva sana mpaka kupoteza nguvu. Ni vizuri pia kula mboga mbichi kama salad (unaweza kuiita kachumbari vyovyote ujuavyo) si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza kuchanganya matango, nyanya na maparachichi au vitunguu saumu, giligilani na karoti. Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukila na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku sio mzuri kwasababu huchangia kunenepa . PENDEKEZO: Unaweza kula ugali kwa samaki, mboga za majani, matango na nyanya bila kuweka chumvi nyingi. 2. Kunywa maji kwa wingi. (glasi 8-10 kwa siku)
Maji ni kinywaji asilia na muhimu sana kwa afya yako, usipende kunywa sana soda au vinywaji vyenye sukari nyingi. Wengi wetu hupendelea kunywa zaidi chai au soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Redull nk). Vinwaji vingi jamii ya soda vina gesi ambayo sio nzuri kwa afya yako kwasababu huongeza uwezekano wa mtu kupata vidonda vya tumbo. Kunywa maji lita 2 kwa siku na pia unashauriwa kunywa maji dakika 10-20 kabla ya kula chakula au nusu saa kuendelea baada ya kupata chakula. Ni kwasababu u takapokunywa maji kabla ya chakula itakusaidia kutokula chakula kingi kupita kiasi kwakuwa utakuwa umeshiba hivyo utaepukana na kula sana ambapo kunaweza kukuongezea uzito wa mwili na hasa kunenepa. Wakati wa kula chakula usinywe maji kwa kubugia harakaharaka hata kama una kiu kali ya maji. Hii ni kwasababu unapokula chakula huku unabugia maji unapunguza nguvu y a chakula, unajaza tumbo maji na kuchelewesha mmeng’enyo wa chakula (digestion). Chakula kisipomeng’enywa vizuri kitaketi tu tumboni. Matokeo yake hali hii ikiendelea kwa muda mrefu itakusababishia kitambi uonekane na tumbo kubwa ambalo si zuri. Kama hutofanya mazoezi ya kusawazisha mwili wako hasa tumbo, hali hii itasab abisha tumbo kwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo na kuleta maradhi kama kisukari, kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbo nakadhalika. 3. Tafuna chakula vizuri.
Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa mdomoni. Mate ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia chakula bila kutafuna sawa sawa unasababisha mambo mawili. Moja chakula kutochambuliwa vizuri na pili chakula kwenda kukaa tumboni bila kutumika au kama kikipita hakitatumika ipasavyo mwilini. Tafuna chakula taratibu na kwa uhakika ili kusaidia umeng’enyaji mzuri kwa matumizi ya mwili. Ukitafuna chakula vizuri pia utakuwa unajiepushia matatizo kama ya kuvimbiwa, kupata choo kigumu nakadhalika. 4. Punguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi.
Mafuta yanahitajika kwa kiasi mwilini, ni vyema ukala vyakula vyenye mafuta kwa mpangilio mzuri unaohitajika mwilini. Kula vyakula kwa kuuwianisha viwango sahihi vya vyakula hivyo (Eat a Well Balanced Diet which Contain Foods at Right Proportion) . Chakula bora kilichokamilika hujumuisha wanga (mfano ugali, ndizi, wali, viazi, mikate, mahindi, nk), protini (mfano mboga na nyama), madini (mfano mbegu mbegu mbichi ambazo hazija kaangwa sana, chumvi nk) na “vitamini” (matunda, maziwa, mayai, nk). Nyama ni muhimu sana kwasababu ina madini aina ya chuma (hasa kwa nyama nyekundu), protini, mafuta na pia inaongeza nguvu. Ila mafuta yaliyoko katika nyama si mazuri kwasababu huganda mwilini. Unashauriwa kula zaidi nyama ya samaki kwakuwa mafuta yake ni mazuri na yana Omega-3 fattyacids ambayo husaidia kuongeza kinga ya maradhi mwilini na pia ni chakula bora kwa afya ya ubongo wako. PENDEKEZO: Kula korosho, karanga (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi kidogo) kuliko nyama kwasababu mafuta yake ni yenye rotuba kuliko mafuta ya kwenye nyama vilevile hayawezi kukuongezea unene. 5. Fanya mazoezi ya mwili na viungo.
Mazoezi ni njia nzuri san a na ya pekee ya kupunguza unene, fanya mazoezi ya kukufanya moyo uendo mbio (cardio excercises) kama kukimbia, kuogelea, kuendesha baiskeli nk yatakusaidia kuchoma na kuyayusha mafuta mwilini. Ni vyema ukafanya mazoezi mpaka mwili utokwe na jasho kwani hiki ni kipimo kizuri cha kudhihirisha umefanya zoezi kwa kiwango stahiki na umeondoa sumu na taka nyingine mwilini. Kama wewe ni mwanachama na unahudhuria GYM kwenda kufanya mazoezi nakushauri uwe na mshirika wa kuwa unafanya naye mazoezi, mkiwa wawili au hata watatu sio mbaya kwa pamoja mtashindana kufanya mazoezi vizuri na ipasavyo . Vilevile mta peana moyo kuendelea na mazoezi yenu kila ito k eapo mmoja wenu anajihisi kukata tamaa. M fano mzuri zaidi wa namna ya kufanya ma zoezi ukiwa nyumbani t umia dakika 10 kuangalia hiyo video clip hap o chini , inaonyesha nam na ya kufanya mazoezi ipasavyo yatakayokusaidia kuchoma calories mwilini ili kupunguza unene na uzito wa mwili . 6. Jiwekee malengo thabiti ya kutaka kupunguza unene. Kupunguza mwili na kuona mabadiliko sio jambo la muda mfupi, linahitaji uvumilivu na subira hasa pale unapokaribia kukata tamaa. Zingatia ulaji bora wa mlo wako wa kila siku na fanya mazoezi ipasavyo bila kuchoka au kuzembea. Ni vyema ukawa na notebook ya kuandika chini maendeleo yako. Mfano unaweza kujiwekea malengo ya kupunguza kilo 1 kila baada ya wiki , n i vyema ukashikilia msimamo wako mpaka ufanikiwe ufikie mahali ujion e na kujiridhisha kwa kujipima ukubwa wako wa sasa na kulinganisha na vipimo vyako vya zamani. Kwa hay o macha che naamini ukiyaf anyia kazi yatakusaidia kupunguza unene wa mwili wako na kuwa mwenye umbo zuri la kuvutia. Kila la heri na nakutakia afya njema !... Makala nyingine za kupitia: Namna ya kutunza afya ya akili na mwili wako. 5 lessons from succesful people. Njia za kukusaidia kumudu kufanya kazi na watu wanaokwamisha shughuli zako. Kama una chochote cha kuongeza kuhusiana na mada hapo juu, tafadhali usisite kutoa maoni yako!
MBINU ZA KUSOMA NA KUFAULU MITIHANI DARASANI.
Kusoma kwa bidii ni moja ya sababu kubwa inayomfanya mwanafunzi kufanya vizuri shuleni, licha ya kuongeza bidii kwenye masomo yako kuna mambo mengine ambayo tumezoea kuyaweka pembeni lakini nayo pia wewe kama mwanafunzi ukiyazingatia mambo hayo yatakusaidia kusoma vizuri zaidi na kuongeza ufaulu wako darasani au kwa sisi tulio vyuoni itakusaidia kuongeza GPA yako kuwa ya 3.8 na zaidi. Mimi binafsi nazitumia hizi mbinu na nimefanikiwa kwa kiasi fulani. Ni vyema nawe ukajaribu uone mabadiliko:
1. Tafuta mahali pazuri pa kusomea. (Zingatia ukimya na utulivu)
-Sehemu ya kusomea nayo ni chanzo kikubwa cha uelewaji wako wakati wa kusoma. Ni vizuri ukikaa mahali ambapo hakuna kelele au muingiliano wa sauti. Ni muhimu kuwe kimya kwani kutakuongezea umakini katika kusoma. Kama unasomea ndani ya chumba maalum hakikisha madirisha yapo wazi kuruhusu hewa kuingia, muhimu hapa ni kusoma mahali ambapo utakuwa huru hakuna kelele, upepo mkali au usumbufu wa aina yeyote.
2. Muhimu kujua unataka kusoma nini na kwa kina gani.
-Kabla ya hujaanza kusoma ni vyema ukajua unataka kusoma nini kwa muda huo, ni kwa kiasi gani unataka uchimbe na kuelewa unachotaka kusoma (do you want to read deep or just shallow). Kusoma kwa kuzingatia mipaka ya unachosoma kutakusaidia usitoke au kwenda mbali na malengo yako ya kile unachotaka kusoma. Kama unasomea mtihani ni vyema ukamuuliza mwalimu wako atatoa mtihani katika mipaka gani ili ujue wapi unatakiwa usome na kutilia mkazo. Angalia pia curriculum ya masomo yako ujue unatakiwa ufahamu mambo gani, hii itakusaidia usome kwa malengo na kujua unatakiwa kuelewa nini kabla ya kuletewa mtihani.
3. Zima simu au iweke kimya (silence) mbali kabisa na mahali unaposomea.
-Moja ya vitu vinavyosababisha upoteze shabaha ya malengo yako ya kusoma ni matumizi ya simu wakati ukisoma. Ukiwa na simu karibu ni rahisi kuchat au kuongea na wako rafiki kwenye simu bila kujua huo si muda sahihi wa wewe kufanya hivyo. Epuka kufanya mambo mengine kinyume na malengo yako ya kusoma kwa muda huo. Nidhamu ni muhimu sana katika kusoma.
4. Waambie watu unahitaji muda wako binafsi wa kufanya mambo yako.
-Kama unakaa nyumbani au hostel na watu wengi, ni rahisi watu kukusumbua wakati unasoma. Ni heri ukawaambia waheshimu muda wako wa kusoma ili kuepusha usumbufu wa hapa na pale utakaokuharibia muda wako maalum wa kusoma. Kama unatumia saa 2 kusoma hakikisha unatumia muda huo kweli kusoma na sio mambo mengine. Jifunze kusema ''HAPANA'' unapoona mtu mwingine anataka kukupotezea muda wako wa thamani. Ikiwezekana waambie hutopatikana hadi saa fulani ili wakutafute baadae kama wanashida na wewe.
5. Tumia saa yako vizuri.
-Panga muda maalum wa kusoma, licha ya kuwa na ratiba ya kawaida ya darasani kuwa na ya kwako binafsi (private study timetable) ujisomee kila unapopata nafasi. Kama utaanda ratiba rasmi ya kujisomea basi inapendekezwa utumie dakika 30-45 kusoma kisha pumzika kwa dakika 5-10. Usisome sana mpaka ukachoka kufikia macho kuchoka au kichwa kuuma, (read smart and not so hard to make you feel pain). Ndio maana ni muhimu kusoma na kupumzika. Wewe sio mashine bali ni binadamu unahitaji kupumzika kidogo na kuendelea na kazi.
6. Wakati wa kusoma, jitahidi kuondoa mawazo nje ya kile unachosoma. Ukihisi umechoka pumzika kwa kuvuta pumzi ili ukusanye nguvu ya kusoma tena.
-Jitahidi kutowaza mambo mengine wakati unasoma isipokuwa yale yanayohusiana na kile unachosoma.Jitahidi sana kuweka mawazo yako darasani uwapo darasani, mimi napenda kuutumia huu msemo ''wherever you are be there''.
7. Pata muda wa kutosha kupumzika kwa kulala muda wa kutosha.
-Wataalamu wa afya wanashauri ulale kiasi cha saa 6 hadi 8 kwa siku kwa ubora wa afya yako. Kwa kulala kiasi cha muda huo utaupa nafasi mwili hasa ubongo wako, kujikarabati na kupata nguvu upya ya kuendelea na kazi uamkapo asubuhi. Pia ni vizuri ukijiwekea muda maalum wa kila siku wa kulala na wa kuamka ili mwili wako uzoe hali hiyo. Kuna tabia ambayo hata mimi nilipokuwa A-Level nilikuwa naifanya kimakosa ya kutotumia muda vizuri wakati wa mchana na kukesha usiku. Mchepuo niliokuwa nasoma ni PCB kweli masomo ni magumu naweza sema kwa wadogo zangu walioko O-level na A-level jitahidini kusoma sana na kutumia muda wenu vizuri hasa mchana ili usiku angalau upate muda wa kulala angalau masaa matano(5) yani unaweza ukalala saa 7 usiku na kuamka saa 12 asubuhi na mapema. Kama ukilala masaa hayo matano vizuri kabisa basi utakuwa umeupumzisha mwili wako (sleep of good quality ensures good health).
8. Soma mambo mbalimbali yanayohusu masomo yako kwenye vitabu au mahali popote. (maktaba au intanet)
-Siku hizi kuna vitabu tele na zana nyingi mbalimbali za kupata maarifa ni wewe tu na muda wako. Tafuta mambo kwenye intanet soma sana, kama shuleni au chuoni kwenu kuna maktaba karibu ingia na usome. Jua mambo mengi (general knowledge) ipo siku utakuja kuona faida yake.
9. Hudhuria vipindi vya masomo (lectures) zote za siku na fanya kazi zote mwalimu atakazowapa.
-Kuwepo kwako darasani kutakuwezesha kutopitwa na mambo mengi darasani. Usikose vipindi bila sababu, na hata kama ukipata dharura ni vyema kila utakapopitwa na kipindi cha somo fulani fanya mpango upate notes mapema usome na kuelewa ili usiachwe nyuma na wenzako. Fanya assignments na discussion za kutosha, wewe huwezi jua mambo yote kuna mambo utakuwa unajua wengine hawajui na mengine hujui wengine wanajua hivyo shirikiana na wenzako.
- See more at: http://kamotta.blogspot.com/2013/07/mbinu-za-kusoma-na-kufaulu-mitihani.html#.SOpctkfTSdk
Jitibu kuzuia tatizo la kuwahi kufika kileleni Ukiwa Nyumbani.
*Mbegu za vitunguu vya kijani (Green onion seed) zina uwezo mkubwa wa kutibu hali ya kuwahi kufika kileleni mapema, jinsi yakutumia chukua Glasi ya maji na uweke kijiko kimoja cha mbegu hizi kisha koroga na unywe kila siku Glasi moja kabla ya kula kila mlo.
*Maziwa ya Almond ni njia nzuri sana ya kutibu hali ya kuwahi kufika kileleni, jinsi ya kufanya chukuwa mbegu kumi za Almond na uziloweke kwenye maji usiku mzima, kisha towa maganda, kisha tia mbegu zilizotolewa maganda ndani ya blenda, changanya na glasi moja ya maziwa ya moto, na pinchi moja ya Tangawizi ya unga, Mdalasini na Hiliki saga pamoja kwenye blenda na unywe mchanganyiko huu kila asubuhi.
*Kufanya Massaji kwenye eneo karibu na prostate Gland hili ni eneo lililopo kati ya korodani na eneo la haja kubwa pia ni ya msaada mkubwa sana, tumia mafuta ya castor kuchua eneo hilo kwa mwendo wa kuzunguka na kugonga taratibu kila siku.
*Unywaji wa Pombe kupindukia na uvutaji wa sigara ni moja ya sababu zinazomfanya mtu kuwahi kufika kileleni hivyo basi uonapo dalili hizi ni vyema kuacha unywaji na uvutaji sigara mapema sana.
*Jumuisha katika kila mlo wako vyakula vya mazao ya bahari kama Samaki, Shellfish, Pweza na Tangawizi, hivi ni vizuri sana katika kuongeza nguvu ya afya ya uzazi na jimai.
*Chemsha Glass moja ya maziwa na uchanganye na kipande kimoja cha Tangawizi na kijiko kimoja cha chai cha Asali Sieve the mazima kisha kunywa kila siku hii pia ni dawa nyingine ya kupunguza hali ya kuwahi kufika kileleni ambayo unaweza kuiandaa ukiwa nyumbani.
*Pendelea kula mara kwa mara vitu asilia vya aina ya aphrodisiacs kama vile nidzi, celery, fennel, carrots, na vitunguu ili kuweza kudhilibiti hali ya kuwahi kufika kileleni.
*Kula punje ama vikonyo vya kitunguu Swaumu kila siku pia ni nzuri kwa Upande huo wa kudhibiti tatizo hili na husaidia kuongeza Ashki ya tendo la ndoa.
*Jifunze jinsi juu ya mazoezi ya kupumua na vuta Taswira (kufanya Meditation), kama nilivyoainisha kwenye maelezo ya awali hali ya kuwahi kufika kileleni huchangiwa wakati mwingine na kuathirika kisaikolojia na hivyo kijifinza kufanya mbinu hizi zitakusaidia utulivu wa Akili na mtazamo makini wa mbeleni. Mawazo na Msongo huchangia tatizo hili hivyo Meditation itasaidia kuondokana na tatizo.
*Maziwa ya Almond ni njia nzuri sana ya kutibu hali ya kuwahi kufika kileleni, jinsi ya kufanya chukuwa mbegu kumi za Almond na uziloweke kwenye maji usiku mzima, kisha towa maganda, kisha tia mbegu zilizotolewa maganda ndani ya blenda, changanya na glasi moja ya maziwa ya moto, na pinchi moja ya Tangawizi ya unga, Mdalasini na Hiliki saga pamoja kwenye blenda na unywe mchanganyiko huu kila asubuhi.
*Kufanya Massaji kwenye eneo karibu na prostate Gland hili ni eneo lililopo kati ya korodani na eneo la haja kubwa pia ni ya msaada mkubwa sana, tumia mafuta ya castor kuchua eneo hilo kwa mwendo wa kuzunguka na kugonga taratibu kila siku.
*Unywaji wa Pombe kupindukia na uvutaji wa sigara ni moja ya sababu zinazomfanya mtu kuwahi kufika kileleni hivyo basi uonapo dalili hizi ni vyema kuacha unywaji na uvutaji sigara mapema sana.
*Jumuisha katika kila mlo wako vyakula vya mazao ya bahari kama Samaki, Shellfish, Pweza na Tangawizi, hivi ni vizuri sana katika kuongeza nguvu ya afya ya uzazi na jimai.
*Chemsha Glass moja ya maziwa na uchanganye na kipande kimoja cha Tangawizi na kijiko kimoja cha chai cha Asali Sieve the mazima kisha kunywa kila siku hii pia ni dawa nyingine ya kupunguza hali ya kuwahi kufika kileleni ambayo unaweza kuiandaa ukiwa nyumbani.
*Pendelea kula mara kwa mara vitu asilia vya aina ya aphrodisiacs kama vile nidzi, celery, fennel, carrots, na vitunguu ili kuweza kudhilibiti hali ya kuwahi kufika kileleni.
*Kula punje ama vikonyo vya kitunguu Swaumu kila siku pia ni nzuri kwa Upande huo wa kudhibiti tatizo hili na husaidia kuongeza Ashki ya tendo la ndoa.
*Jifunze jinsi juu ya mazoezi ya kupumua na vuta Taswira (kufanya Meditation), kama nilivyoainisha kwenye maelezo ya awali hali ya kuwahi kufika kileleni huchangiwa wakati mwingine na kuathirika kisaikolojia na hivyo kijifinza kufanya mbinu hizi zitakusaidia utulivu wa Akili na mtazamo makini wa mbeleni. Mawazo na Msongo huchangia tatizo hili hivyo Meditation itasaidia kuondokana na tatizo.
KAROTI KINGA DHIDI YA SARATANI NA UGONJWA WA MOYO
Kwa ujumla wake, karoti ni mboga yenye kiasi kingi cha Vitamin A. Mbali ya vitamini hiyo, karoti ina virutubisho vingine muhimu vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa hatari, kama vile saratani, moyo na mengine mengi na kumbuka kwamba; ‘kinga ni bora kuliko tiba’.
Sifa pekee na kubwa kuhusu karoti inayojulikana na watu wengi, ni uwezo wake wa kuimarisha nuru ya macho na uwezo wa kuona, hususan wakati wa usiku. Katika makala ya leo nitakufahamisha faida nyingine za mboga hii rahisi, inayopatikana kwa wingi, mijini na vijijini. Ukiielewa vizuri, itaokoa maisha yako.
VIRUTUBISHO VYA KAROTI
Kwa mujibu wa tafiti kadhaa zilizofanywa, imethibitika kuwa karoti ina kiwango kikubwa cha virutubisho jamii ya ‘carotenoids’ ambavyo husaidia sana kuupa mwili uwezo wake wa asili wa kupambana na maradhi yanayojitokeza mwilini.
Aina Mbili Ya Vyakula Hutakiwi Kuvila Baada Ya Mazoezi
KAMA
wewe ni miongoni mwa watu wenye utaratibu wa kufanya mazoezi ya mwili kila siku
au mara kwa mara unahitaji kusoma makala haya kwa makini, kwani yanahusu suala
muhimu ambalo pengine hukuwahi kulijua kabla.
Inaeleweka na kukubalika na tafiti zote kuwa mazoezi ya mwili ni miongoni mwa vitu muhimu kiafya kufanywa na mtu
Inaeleweka na kukubalika na tafiti zote kuwa mazoezi ya mwili ni miongoni mwa vitu muhimu kiafya kufanywa na mtu
baada ya kuzingatia lishe. Imeelezwa pia
kwamba mazoezi yanachukua asilimia 20 ya ustawi wa afya ya mtu, hii ina maana
kwamba hata kama utakula vyakula sahihi, kama hufanyi mazoezi, ubora wa afya
yako utakuwa haujakamilika kwa asilimia 20.