Home » Posts filed under Mapenzi
Showing posts with label Mapenzi. Show all posts
Showing posts with label Mapenzi. Show all posts
MAADILI YANAZIDI KUPOROMIOKA, AGESS APIGA TENA PICHA ZA UTUPU NA KUZIACHIA MTANDAONI
Masogange na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakidhaniwa kuwa na madawa haramu ya kulevya na baadaye mahakama kuu ya nchini humo ikawaachia kwa dhamana ikidai unga waliokutwa nao si madawa ya kulevya bali ni mali ghafi zijulikanazo kama Methamphetamine.
“Sasa huu upuuzi gani unatuwekea humu, kwani kila kitu unachofanya ni lazima sisi tuone? Hivi kwa nini mastaa wa Bongo wanapenda kujirahisi kiasi hiki?” alihoji mmoja wa wafuasi wa mtandao huo.
Pamoja na wadau wengi kuonesha kukerwa na picha hizo, Masogange hakujali, aliwajibu kuwa kama hawataki kuziona picha hizo wamuondoe kwenye listi ya marafiki mtandaoni humo kwani siyo lazima.
“Hii ni akaunti yangu, nina uhuru wa kuweka picha za aina yoyote. Kama mtu anaona nimemkera basi ‘aniblok’ maana hapa nimevaa mavazi ya kuogelea sasa mlitaka nivae pensi niogelee nayo? Simuogopi mtu…,” aliandika Masogange.
JE? UNAHISI MPENZI WAKO ANAKUSALITI? ZIJUE SABABU NA TIBA YA USALITI KATIKA MAPENZI
Unahisi mwenzi wako siyo mwaminifu? Kwa jumla ni kwamba, kuna
watu wengi wanaoonekana wazi kuwa siyo waaminifu. Wengine ukiambiwa huyu
ameoa au kuolewa inakupa wakati mgumu kuamini kwa namna anavyoendelea
kufanya mambo ya ngono na watu wengine.
Usaliti ni tabia inayokera mno. Ukisikia mwenzi
wako amesaliti, ni wazi hutakuwa na furaha naye; Utajiuliza mengi, hasa
kutaka kujua sababu na pengine kujua huyo aliyesaliti naye ana kipi
ambacho wewe hauna?
Tendo la kusaliti lina maumivu makali hata
kusababisha wengine kuchukua uamuzi mgumu kama kujiua, kutokula na tabia
nyingine hatarishi zinazofanana na hizo.
Hata hivyo, siyo sahihi kujiua, wala kujiumiza kwa
sababu yoyote ile. Wakati mwingine kuachana na fulani huweza kuwa ni
jambo jema ili kumpata mtu anayefaa zaidi.
Maumivu ya usaliti yanamhitaji mtu kuwa mwangalifu, vinginevyo anaweza kuchukua uamuzi usio na maana kwake, wala maisha yake.
Utajisikiaje akiwa na mwingine, au siku akikuletea mtoto wa nje ya ndoa?
Hakuna shaka kwamba tendo hili linaumiza, kwamba
uko na mtu halafu anakuja na mtoto kutoka nje ya ndoa, au labda unasikia
kwamba ana mwingine. Kwa mtu aliyetenda usaliti, nafsi yake humsuta kwa
kujiona ni mkosaji.
Msingi wa kuwa na maisha bora ni kuhakikisha
unamfanyia mwenzi wako mambo unayopenda wewe kufanyiwa. Hebu fanya kama
vile wewe ni mwenzi wako, jione kama vile unasalitiwa, bila shaka
ungeumia. Ikiwa utaumia, kwa nini unamsaliti mwingine?
Ishi hivi
Penda kufanya mazuri, yale ambayo wewe ungependa
kufanyiwa na mwenzi wako. Penda kuwa na moyo wa huruma, akili yako
ifanye kazi ipasavyo kwa kubuni mambo mazuri ya kufanya kwa mwenzi wako;
Ni suala la kuelewa kuwa msingi wa kuwa na uhusiano mzuri ni kujiona
kana kwamba wewe ni mwenye deni la kumfanyia mazuri mwenzi wako.
Mambo muhimu ya kuzuia usaliti
Kwa sababu baadhi ya watu wamekuwa wakikubali kuwa
na wapenzi wengine kwa shinikizo la kiuchumi, hivyo ni jambo la msingi
kwa watu walio kwenye uhusiano kuangalia njia za kuongeza kipato kupitia
kazi mbalimbali. Wanandoa wanapaswa kubuni miradi ya kufanya, ili
hatimaye suala la kiuchumi lisiwe tatizo.
Iwe ni lazima kwa wanawake na wanaume, wote kuangalia namna ya
kufanya ili kujiongezea kipato; lengo liwe ni kujitosheleza kipato. Siyo
jambo zuri kumtegemea mtu mmoja katika suala la uchumi kwani anaweza
kuugua au labda kuwa na matatizo mengine yoyote ya kazi.
Mwanamke ajiepushe na utegemezi, hii itajenga
upendo wenye heshima na itamwongezea mwanamume kutambua umuhimu wa uwepo
wa mwanamke katika maisha yake.
Mambo mengine ni maarifa juu ya mapenzi na tendo
la ndoa.Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha mwenzi wake anafurahia
mapenzi yenu kwa maana ya kujaliana, kushauriana, kusikilizana na
kuheshimiana. Katika tendo la ndoa, ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha
anajua ashughulike vipi ili kutoshelezana.
Muhimu kuzingatia
a) Wanandoa wanapaswa kuandaana kisaikolojia kabla
ya tendo, kwa mfano kwa kutumiana meseji hasa kama wapenzi hao wako
mbali, kuondoa tofauti zao kwa maana ya migogoro na njia zingine za
kufanya wapenzi kufurahiana.
b) Kuzijua sehemu za hisia za mwenzi wako (sehemu za mwanamke zipo 12 na kwa mwanaume zipo 5)
c) Unadhifu na usafi wa mwili ni jambo muhimu
sana. Ni muhimu pia kuonyesha ushirikiano Fanya ndoa iwe bora; Wanandoa
wanapaswa kuwa marafiki wa karibu. Kama kweli mnataka kuwa na raha
katika ndoa, fanyeni kana kwamba ninyi ni marafiki na siyo mabosi kama
wanavyofanya baadhi ya watu.
Mfanye mwenzi wako awe mshauri na mfariji wako. Uwe mwenye utu; Uwazi, busara, uvumilivu ukizingatia imani ya dini.
HATA KAMA UMZURI, BILA UTUNDU FARAGHA HUNA NYIMBO!
Mapenzi yana kanuni zake, kanuni ambazo usipozifuata huwezi kupata furaha uliyotarajia. Unapotokea kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza lakini omba sana upate ile bahati ya kumpenda mtu ambaye naye anakupenda kwa dhati. Kwa bahati mbaya ukitokea kumzimikia mtu ambaye wala hana hata chembe za penzi kwako, utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye, utakuwa unajitafutia vidonda vya tumbo.
Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata wapenzi wa ukweli lakini kwa kushindwa kwao kujua yapi ya kufanya ili kudumisha penzi, leo hii wameachika na bado wanaranda mtaani.
Kwa kifupi ni kwamba, unapoingia kwenye uhusiano na mtu na ukabaini naye anakupenda, hutakiwi kubweteka bali unatakiwa kutumia utundu na ubunifu wako katika yale ambayo yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa kipekee kwake.
Ninapozungumzia hayo, namaanisha ubunifu kwenye mambo mengi ambayo hakika nikianza kuyaelezea hapa, nafasi inaweza isitoshe ila kwa leo nigusie utundu na ubunifu katika uwanja wetu ulee wa kujidai.
Faragha ni eneo muhimu sana ambalo linaweza kubomoa au kuimarisha ndoa. Ninapozungumzia hilo, ni kwa wote yaani mke na mume.
Mwanaume anatakiwa kumridhisha mkewe kwa kiwango kinachostahili. Kusiwepo mazingira ya kupeana mambo kiduchu kwani ikiwa hivyo lazima mke atakosa furaha iliyokamilika.
Ila sasa leo nataka niwazungumzie kwa kirefu wanawake. Kuna wanawake ambao wamebahatika kupata wanaume wanaowapenda sana na kuwapatia kila wanachohitaji.
Hawa wanatakiwa kujiona ni wenye bahati kubwa kwani kwa hali ilivyo sasa, wanawake wengi wanatafuta wanaume wa kuwaoa hawawapati.
Kinachonishangaza ni kwamba, kuna baadhi ya wanawake ambao wako ndani ya ndoa lakini wamejisahau kwamba wana jukumu la kuwapa waume zao furaha ambazo hawawezi kuzipata kwingine.
Ukijaribu kuchunguza utabaini wanawake wengi walio ndani ya ndoa licha ya uzuri walionao, siku hizi wanasalitiwa sana.
Hii ni kwa sababu wamekuwa waongeaji mno lakini wanapokuwa faragha unaweza ukadhani siyo wao.
Hawajui kitu, wamekaa kama magogo tu halafu eti wanadhani hawatasalitiwa na ndoa zao zitadumu, zitadumu kwa misingi ipi?
Mwanamke akae akijua kwamba, mumewe ni kama mtoto ambaye anatakiwa kubembelezwa huku akipewa vitu vitamu ili kumpumbaza asishawishike kutoka nje.
Ukiwa kwenye ndoa kisha ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa kuwa tayari ulishapendwa, ipo siku utajikuta ni mke wa pambo la nyumba tu.
Mtaani kuna utitiri wa nyumba ndogo, wanaume walioanzisha makoloni hayo nje ya ndoa zao walikosa wake sahihi ambao wanaweza kuwashikilia.
Matokeo yake sasa nyumba ndogo hizo ndizo zinazoonekana kuwashika waume za watu siku hizi na wanafanikiwa kwa kuwa ni watundu na wabunifu.
Sasa kwa nini wewe mwanamke uliye ndani ya ndoa usifanye yale wanayofanya nyumba ndogo? Je, uko tayari kuachika eti kwa kuwa huoneshi kuwa mzoefu pale faragha unapokutana na mzee?
Hata kama si mjuaji kwenye mambo mengine lakini unatakiwa kujifunza. Waulize watu wenye uzoefu, najua watakufundisha yapi ya kufanya ili kumshika mumeo. Kinyume chake ni kwamba, hata kama umzuri kiasi gani mumeo atakusaliti na unaweza kujikuta unatoswa kabisa.

KINACHOMFANYA MWANAUME AKOROME NA KULALA BAADA YA TENDO LA NDOA NI MAUMBILE NA SIYO HIARI YAKE
Jambo hili huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali chungu mzima kama kuna mahali wamekosea au hawajawavutia wapenzi wao, pale wenzi wao wanapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi punde tu baada ya kumaliza tendo la kujamiiana.
Lakini utafiti uliofanywa hivi na wanasayansi unawapa wanaume ahuweni katika kuepuka lawama hizo, kwamba, kumbe siyo hiyari yao, bali ni maumbile.
Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa sababu za kimaumbile ubongo wa wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi baada ya kushiriki tendo la kujamiiana. Katika utafiti wao wanasayansi hao walibaini kwamba, kwa jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa, pale wanapomaliza tendo la kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo linalozimika na kuwafanya kupata usingizi.
Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali ni tofauti, kwani wao hubaki wakikodolea macho dari wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali lukuki, wakijihisi kutowaridhisha wapenzi wao.
Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha kipimo cha kumulika, maarufu kama scan, ambapo kilitumika kuwamulika wanaume katika ubongo wao pale wanapofanya tendo la kujamiiana na baada ya kumaliza kujamiiana na kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’ huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.
"Utafiti huu unatupa matokeo ya kile kinachotokea ndani ya ubongo pale mwanaume anapofika kileleni.” Gazeti la Mirror lilimnukuu mwanasayansi mmoja wa serikali ya Ufaransa aitwae Serge Stoleru.
“Lakini kwa wanawake inaonekana ni tofauti kabisa……” Aliongeza kusema mwanasayansi huyo.
Mwanasayansi huyo aliendelea kusema kwamba, wanawake hushangazwa sana na jambo hilo na ndio sababu hubaki wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala baada ya kumaliza tendo ilo hali wao wakitaka zaidi….
Kwa hiyo hakuna sababu ya wanawake kuwalaumu tena wanaume baada ya kumaliza tendo na kulala kwa sababu hivi sasa wameshajua sababu, watuache tupumuwe……

MAHABA: MAMBO 5 YA KUEPUKA MARA TU UNAPOCHUMBIWA
Kuna mambo kadhaa ambayo msichana anatakiwa kuwa makini nayo katika kuhakikisha uchumba wako unadumu na kufikia hatua ya kuolewa na kwenda kuanza maisha mapya.
Yapo mengi lakini nitagusia matano ambayo kwa utafiti wangu ndiyo
yamekuwa yakiwafanya wengi wakimbiwe na wachumba wao na kuachwa wakilia.
Mazoea na wanaume
Wapo ambao wamejikuta wakiachwa solemba kufuatia tabia zao za kuwa na mazoea ya kijinga na wanaume.
Yawezekana kabla ya kuchumbiwa marafiki zako wakubwa walikuwa wanaume (Wapo wanawake wa aina hiyo). Unachotakiwa kufahamu ni kwamba hakuna mwanaume anayefurahia ukaribu wa mchumba wake kwa wanaume wengine.
Hata kama hakuna uhusiano wa kimapenzi lakini epuka sana kujichekelesha kwao, kuongozana nao, kukaa nao au hata kuwasiliana nao. Ukifanya hivyo utakuwa unamkwaza mchumba wako na inaweza kuwa moja ya sababu za kukuchenga.
Marafiki micharuko
Ukishachumbiwa, kuna marafiki zako ambao ‘automatikale’ unatakiwa kuachana nao. Nazungumzia wale micharuko ambao hawawezi kukushauri vizuri juu ya maisha yako.
Hata wale ambao wamekuwa wakikushawishi kila wikiendi muende mkajirushe, baada ya kuchumbiwa unatakiwa kujiweka mbali nao ili kumpa amani mchumba wako.
Tabia za kisichana
Ukishachumbiwa wewe si msichana tena, utakuwa ni mama mtarajiwa wa familia yako. Tabia za kisichana kama vile kuvaa mavazi yasiyo ya heshima, kukaa vijiweni kuongea mambo ya umbeya na nyinginezo kama hizo hutakiwi kuendelea kuwa nazo.
Kujifanyisha
Alichokupendea huyo mchumba wako anakijua mwenyewe, kwa maana hiyo unatakiwa kuendelea kubaki wewe kama wewe. Usijifanyishe kwa namna yoyote kama ambavyo baadhi ya wasichana wamekuwa wakifanya.
Eti umeshaolewa
Kuolewa ni mpaka pale mtakapoingia kanisani, msikitini nk na kufungishwa ndoa. Kama bado hamjafika huko, wewe bado ni mchumba tu na hata kwenye ndoa unaweza usifike.
Kwa maana hiyo hutakiwi kuhamia kwa mwanaume kama ambavyo baadhi wamekuwa wakifanya. Unachotakiwa kufahamu ni kwamba kitendo cha wewe kuchumbiwa kisha kuamua kubeba virago vyako na kwenda kuishi na mwanaume ni kuwakosea wazazi.
Msomaji wangu, yapo mengi ya kuepuka mara tu unapochumbiwa lakini haya machache yanatosha kwa leo. Jiangalie tabia zako, zile ambazo unajua wanaume wengi haziwafurahishi, jiepushe nazo ili kumjengea mchumba wako mazingira ya kukamilisha taratibu za ndoa yenu.

DALILI ZA MWANAMKE ANAYETOKA NJE YA NDOA
Wataalamu wa maswala ya mahusiano wanaamini kwamba, mwanamke anapotoka nje ya ndoa yake, inakuwa rahisi sana kubainika au kufumaniwa kuliko ilivyo kwa mwanaume.
Hii inatokana na ukweli kwamba, hisia zinakuwa na nafasi kubwa sana kwa mwanamke, kwani mwanamke huishi kwa hisia zaidi kuliko mwanaume. Bado nasisitiza kwamba, haipaswi na siyo sahihi mtu kuchukulia dalili hizi kama ushahidi wa mpenzi wake kutoka nje ya ndoa. Uchunguzi wa kina kufuatia dalili hizi ni muhimu sana.
Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya dalili zinazoweza kuonyeshwa na mwanamke ambaye anatoka au yupo kwenye harakati za kutoka nje ya ndoa yake:
1. KUCHELEWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuaga kwamba anakwenda saluni au kusuka, badala ya kurejea kwa muda ambao umezoeleka, anachukua muda mrefu hata mara tatu zaidi. kuna wakati kwenda sokoni huchukua saa kadhaa bila kujali soko liko umbali gani. Kama ni mara moja sawa, lakini ikishakuwa zaidi ya mara moja huenda kuna tatizo la kukosa uaminifu.
2. KUBADILI MAENEO: Hebu chukulia kwamba, mwanamke amezoea kwenda soko fulani la karibu, hospitali fulani ya karibu, saluni fulani ya karibu na hata nyumba fulani ya ibada ya karibu. Unapoona anahama maeneo ya karibu ya huduma na kwenda ya mbali, bila sababu ya msingi, huna budi kuanza kutuhumu mwenendo mbaya.
Siyo lazima kuhama kokote kuwe na mwenendo mbaya, lakini kama kuhama kwenyewe kunatia shaka kwa sababu maelezo ya kuhama huko hayana msingi, mwanaume ana kila sababu ya kuchunguza kama hakuna usaliti unaofanywa.
3. UNUNUZI USIO WA KAWAIDA: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake kwa ajili ya kupata fedha, basi atakuwa na mabadiliko makubwa katika mtindo wake wa manunuzi.
Atakuwa ananunua vitu vya thamani kubwa kuliko uwezo wake, atakuwa na fedha nyingi tofauti na ambazo angekuwa nazo na pengine kumiliki mali kama nyumba kwa siri.
4. KUANZISHA VURUGU: Kuna wakati mwanamke anayetoka nje ya ndoa huanzisha vurugu za makusudi na mumewe. Lengo la kuanzisha vurugu hizo ni ili apate nafasi ya kujifanya amezira na kuondoka nyumbani kwa muda.
Huo muda anapoondoka nyumbani kujifanya kakerwa na vurugu hizo ndiyo muda ambao anautumia kwenda kwa hawara yake.
5. KUSITISHA UAMINIFU: Mwanamke anayetoka nje ya ndoa, mara nyingi husimamisha kumwamini mumewe, yaani hayuko tayari kushiriki masuala ya siri, ambayo wanandoa huwa wanashiriki.
Husita kumshirikisha mumewe kwenye mambo yake mengi. Lakini pia husita kumuomba mumewe ushauri, kama alivyokuwa akifanya siku za nyuma.
6. KUACHA KUVAA PETE: Kuna sababu nyingi ni kwa nini mwanamke anaweza kuacha kuvaa pete yake ya ndoa. Moja ya sababu hizo ni kusalitiwa na mumewe au ndoa yake kuwa kwenye misukosuko mikubwa sana.
Lakini nje ya misukosuko mikubwa ya ndoa, sababu nyingine inayoweza kumpelekea mwanamke kuvua mara kwa mara au moja kwa moja pete yake ya ndoa, ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa yake.
7. KUONESHA WASIWASI: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake , ni lazima atakuwa na wasiwasi na mashaka yasiyo na sababu mbele ya mume wake.
Anaweza kuonesha kutotulia kwa aina fulani kana kwamba, anahofia kuna siri itatoka au kuna kitu ambacho tayari mume wake anakijua dhidi yake. Mara nyingi wasiwasi na mashaka humtawala sana mwanamke anayetoka nje , hasa katika hatua zake za awali za kutoka nje.
8. KUZUNGUMZIA KUACHWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuwa anatoa kauli za kuonesha kwamba, kama mwanaume anaona vipi , wanaweza kuachana.
Kama kila penye ugomvi kidogo tu mwanamke anakimbilia kusema, “kama ni kuachana, tuachane tu” hiyo inaweza kuwa ni dalili mbaya kwa mwanamke anayetoka nje ya ndoa kwa sababu hana tena upendo na mumewe