UNATAKA KUFANIKIWA? HAKUNA NJIA YA MKATO KATIKA MAFANIKIO
Je huu ni ukweli kwamba hakuna njia ya mkato kuelekea
mafanikio? Inawezekana unasema ‘Awali hujui mambo yanayoendelea na utabakia
hivyo hivyo’. Kuna kitu nimeendelea kujifunza kwa watu matajiri wanaochipukia
kwenye Forbes magazine na kwingineko.
Siku chache zilizopita katika Kongamano fulani ambako
Mjasiriamali wa Kenya Julian Kyula na Heshan De Silva waliongea kutokana na
uzoefu na historia ya Maisha yao. Kitu kimoja cha kufanana ni kutumia kile
ulichonacho na uweze kukiendeleza kufikia kule unakotaka.
Hakuna Njia ya Mkato kwenye Mafanikio; Kama kuna kitu
ambacho hatutaweza kuendelea ni kupitia njia za mkato. Njia za mkato haziwezi
kujenga maendeleo yako wala hutoweza kuacha kitu kiuchumi. Kwanini? Kuwa na
fedha ambayo huna maelezo nayo au haujaiwekeza kwenye njia sahihi ni kupoteza
hiyo mali.
Mimi huangalia zaidi upande chanya zaidi kuliko upande hasi,
kwa kila mtu ambaye namtolea mfano naangalia upande chanya, kama una kitu hasi
juu ya yeyote huo sio upande wangu wa makala hii.
Kuna njia nyingi za utafutaji wa mafanikio “kama kupanda na
kuvuna” kitu ambacho watu wengi wanapenda, vilevile biashara za njia ya
mitandao ili upate kamisheni kwaajili ya watu wanaojiunga chini yako. Hizo
hazijawahi kuwa njia sahihi za kufanikiwa mara nyingi zinaishia kutapeliwa.
Kufanya kazi kwa umakini na sio kwa nguvu. Umakini
unaozungumziwa hapa ni kuwa na watu sahihi au mtandao sahihi wa watu kuhusu
biashara au bidhaa unayoifanya. Umakini huo utakusaidia kufikia malengo yako,
haimaanishi kwamba hautakutana na vikwazo mbalimbali ila je una umakini gani
kupambana na vikwazo hivyo?
Inabidi Ukuze kitu ulichonacho. Watu wengi tunaogopa
kuchukua hatua ya kuamini kwamba kitu ulichonacho kinaweza kuwa kitu kikubwa
cha kuweza kukutengenezea ajira yako na watu wengine. Tunakuwa na sababu nyingi
na za kutosha kuonyesha kwamba haiwezekani. Ila ukweli uko hivi kwako
haiwezekani ila kuna mtu sehemu fulani usiyoijua wewe kimewezekana. Hivyo
inategemea mtazamo wako ukoje. Vitu vingi tunavyovifanya sasa hivi wazee wetu
hawajawahi kufikiri kwamba vitawezekana lakini vinafanyika na wanaona vinawezekana,
hivyo badilisha unavyofikiri unaweza ukabadiisha matokeo ya vitu unavyofanya
kila siku. Nuia Kukua kimtizamo na kiutendaji.
0 comments: