MBINU ZA KUSOMA NA KUFAULU MITIHANI DARASANI.

Kusoma kwa bidii ni moja ya sababu kubwa inayomfanya mwanafunzi kufanya vizuri shuleni, licha ya kuongeza bidii kwenye masomo yako kuna mambo mengine ambayo tumezoea kuyaweka pembeni lakini nayo pia wewe kama mwanafunzi ukiyazingatia mambo hayo yatakusaidia kusoma vizuri zaidi na kuongeza ufaulu wako darasani au kwa sisi tulio vyuoni itakusaidia kuongeza GPA yako kuwa ya 3.8 na zaidi. Mimi binafsi nazitumia hizi mbinu na nimefanikiwa kwa kiasi fulani. Ni vyema nawe ukajaribu uone mabadiliko:

1. Tafuta mahali pazuri pa kusomea. (Zingatia ukimya na utulivu)
-Sehemu ya kusomea nayo ni chanzo kikubwa cha uelewaji wako wakati wa kusoma. Ni vizuri ukikaa mahali ambapo hakuna kelele au muingiliano wa sauti. Ni muhimu kuwe kimya kwani kutakuongezea umakini katika kusoma. Kama unasomea ndani ya chumba maalum hakikisha madirisha yapo wazi kuruhusu hewa kuingia, muhimu hapa ni kusoma mahali ambapo utakuwa huru hakuna kelele, upepo mkali au usumbufu wa aina yeyote.

2. Muhimu kujua unataka kusoma nini na kwa kina gani.
-Kabla ya hujaanza kusoma ni vyema ukajua unataka kusoma nini kwa muda huo, ni kwa kiasi gani unataka uchimbe na kuelewa unachotaka kusoma (do you want to read deep or just shallow). Kusoma kwa kuzingatia mipaka ya unachosoma kutakusaidia usitoke au kwenda mbali na malengo yako ya kile unachotaka kusoma. Kama unasomea mtihani ni vyema ukamuuliza mwalimu wako atatoa mtihani katika mipaka gani ili ujue wapi unatakiwa usome na kutilia mkazo. Angalia pia curriculum ya masomo yako ujue unatakiwa ufahamu mambo gani, hii itakusaidia usome kwa malengo na kujua unatakiwa kuelewa nini kabla ya kuletewa mtihani.

3. Zima simu au iweke kimya (silence) mbali kabisa na mahali unaposomea.
-Moja ya vitu vinavyosababisha upoteze shabaha ya malengo yako ya kusoma ni matumizi ya simu wakati ukisoma. Ukiwa na simu karibu ni rahisi kuchat au kuongea na wako rafiki kwenye simu bila kujua huo si muda sahihi wa wewe kufanya hivyo. Epuka kufanya mambo mengine kinyume na malengo yako ya kusoma kwa muda huo. Nidhamu ni muhimu sana katika kusoma.

4. Waambie watu unahitaji muda wako binafsi wa kufanya mambo yako.
-Kama unakaa nyumbani au hostel na watu wengi, ni rahisi watu kukusumbua wakati unasoma. Ni heri ukawaambia waheshimu muda wako wa kusoma ili kuepusha usumbufu wa hapa na pale utakaokuharibia muda wako maalum wa kusoma. Kama unatumia saa 2 kusoma hakikisha unatumia muda huo kweli kusoma na sio mambo mengine. Jifunze kusema ''HAPANA'' unapoona mtu mwingine anataka kukupotezea muda wako wa thamani. Ikiwezekana waambie hutopatikana hadi saa fulani ili wakutafute baadae kama wanashida na wewe.

5. Tumia saa yako vizuri.
-Panga muda maalum wa kusoma, licha ya kuwa na ratiba ya kawaida ya darasani kuwa na ya kwako binafsi (private study timetable) ujisomee kila unapopata nafasi. Kama utaanda ratiba rasmi ya kujisomea basi inapendekezwa utumie dakika 30-45 kusoma kisha pumzika kwa dakika 5-10. Usisome sana mpaka ukachoka kufikia macho kuchoka au kichwa kuuma, (read smart and not so hard to make you feel pain). Ndio maana ni muhimu kusoma na kupumzika. Wewe sio mashine bali ni binadamu unahitaji kupumzika kidogo na kuendelea na kazi.

6. Wakati wa kusoma, jitahidi kuondoa mawazo nje ya kile unachosoma. Ukihisi umechoka pumzika kwa kuvuta pumzi ili ukusanye nguvu ya kusoma tena.
-Jitahidi kutowaza mambo mengine wakati unasoma isipokuwa yale yanayohusiana na kile unachosoma.Jitahidi sana kuweka mawazo yako darasani uwapo darasani, mimi napenda kuutumia huu msemo ''wherever you are be there''.

7. Pata muda wa kutosha kupumzika kwa kulala muda wa kutosha.
-Wataalamu wa afya wanashauri ulale kiasi cha saa 6 hadi 8 kwa siku kwa ubora wa afya yako. Kwa kulala kiasi cha muda huo utaupa nafasi mwili hasa ubongo wako, kujikarabati na kupata nguvu upya ya kuendelea na kazi uamkapo asubuhi. Pia ni vizuri ukijiwekea muda maalum wa kila siku wa kulala na wa kuamka ili mwili wako uzoe hali hiyo. Kuna tabia ambayo hata mimi nilipokuwa A-Level nilikuwa naifanya kimakosa ya kutotumia muda vizuri wakati wa mchana na kukesha usiku. Mchepuo niliokuwa nasoma ni PCB kweli masomo ni magumu naweza sema kwa wadogo zangu walioko O-level na A-level jitahidini kusoma sana na kutumia muda wenu vizuri hasa mchana ili usiku angalau upate muda wa kulala angalau masaa matano(5) yani unaweza ukalala saa 7 usiku na kuamka saa 12 asubuhi na mapema. Kama ukilala masaa hayo matano vizuri kabisa basi utakuwa umeupumzisha mwili wako (sleep of good quality ensures good health).

8. Soma mambo mbalimbali yanayohusu masomo yako kwenye vitabu au mahali popote. (maktaba au intanet)
-Siku hizi kuna vitabu tele na zana nyingi mbalimbali za kupata maarifa ni wewe tu na muda wako. Tafuta mambo kwenye intanet soma sana, kama shuleni au chuoni kwenu kuna maktaba karibu ingia na usome. Jua mambo mengi (general knowledge) ipo siku utakuja kuona faida yake.

9. Hudhuria vipindi vya masomo (lectures) zote za siku na fanya kazi zote mwalimu atakazowapa.
-Kuwepo kwako darasani kutakuwezesha kutopitwa na mambo mengi darasani. Usikose vipindi bila sababu, na hata kama ukipata dharura ni vyema kila utakapopitwa na kipindi cha somo fulani fanya mpango upate notes mapema usome na kuelewa ili usiachwe nyuma na wenzako. Fanya assignments na discussion za kutosha, wewe huwezi jua mambo yote kuna mambo utakuwa unajua wengine hawajui na mengine hujui wengine wanajua hivyo shirikiana na wenzako.
- See more at: http://kamotta.blogspot.com/2013/07/mbinu-za-kusoma-na-kufaulu-mitihani.html#.SOpctkfTSdk

0 comments:

Post a Comment

Recent Posts