Home » Posts filed under Habari za Kitaifa
Showing posts with label Habari za Kitaifa. Show all posts
Showing posts with label Habari za Kitaifa. Show all posts
Maharusi waoana ndani ya bwawa la maji
Maharusi wawili walifanya harusi yao katika bwawa lenye lita milioni 1.5 za maji ya bahari .
Bwawa hilo hutumiwa kutoa mafunzo ya kupiga mbizi katika kituo cha Fort William.Bi Dorota Bankowska mpiga mbizi mzoefu aliolewa na mpenzi wake ambaye ni mwalimu James Abbot nyumbani kwao mjini Plock , Poland mwezi jana lakini akataka sana kufanya jambo la kipekee wanakoishi kama ishara ya kusherehekea harusi yao.
Bi Abbott alipokea mafunzo ya upigaji mbizi katika kituo hicho kilicho katika ufuo wa bahari ya Loch Linnhe mnamo mwaka 2007 na kuwaomba wafanyakazi wa kituo hicho wamruhusu afanye harusi yake chini ya maji hayo.
Bwawa hilo, hutumiwa kutoa mafunzo kwa wapiga mbizi pamoja na kufanyia majaribio vifaa vipya. Picha hizi zimetolewa na kituo hicho.
Bi harusi alivalia gauni nyeupe huku bwana harusi akivalia sketi ambayo huvaliwa na waskochi ijulikanao kama 'Kilt'.
Maharusi hao waliungana na marafiki wao Ala Bankowska na Charlie Cran-Crombien chini ya maji hayo.
Wote wanne walivalia vifaa vya kupigia mbizi pamoja na mavazi yao ya harusi.
Takriban wageni 100 walitazama harusi hio wakiwa nje
Bi Abbott anafanya kazi katika kiwanda cha mafuta na gesi.
Rapper Navio ambaye yupo Bongo asema anatamani kufanya collabo na Izzo Bizness
“Humbled…Hii kubwa sana kwangu”, ni maneno aliyoyasema
rapper Izzo Bizness kuelezea furaha yake baada ya kumsikia rapper mkubwa wa
Uganda Navio akimtaja kwenye radio kuwa angependa kufanya naye collabo.
Navio yupo Tanzania, na jana (Nov.18) alifanyiwa mahojiano
kwenye kipindi cha Power Jams kupitia East Africa Radio. Alipoulizwa wasanii wa
Bongo ambao anatamani kufanya nao collabo, miongoni mwao alimtaja rapper Izzo
Bizness.
Izzo alipost tweet
yake Instagram na kuandika “Hii kubwa sana kwangu big up kwa #NAVIO
#HAINAKUFELI”
Izzo amezungumza na Bongo 5 kuhusu mpango wa kufanya collabo
na Navio kabla hajaondoka nchini.
“Yeah plan zipo tunataka kufanya ngoma, tulikuwa turekodi
jana lakini kutokana na ratiba yake ilivyokuwa tight kwaajili ya interviews na
nini mpaka muda aliofika alikuwa tayari kaishachoka tayari kwahiyo akaona
tuisogeze mbele, tujaribu kuwasiliana leo mapema halafu tujue tunafanyaje,
lakini mipango ambayo ipo inabidi tufanye ngoma.”
East Coast Team kuingia kambini kuandaa ngoma mpya, maproducer wanne kuhusika!
East Coast Team inarejea tena. King Crazy GK, AY, Mwana FA, Snare na Buff G, wanatarajia kuingia kambini hivi karibuni kuandaa nyimbo mpya. Maproducer wanne watashiriki kwenye mradi huo.
Wasanii wa East Coast AY, GK, Snare pamoja na Buff G
GK ameimbia Bongo5 kuwa wapo kwenye maandalizi ya mwisho kuingia kambini na kuanza kazi hiyo.
“Tumechagua ma-producer wanne, tumemchagua Marco Chali, tumemchangua John Maundi, Mr T Touch na kuna mwingine mmoja. Producer wote watatengeneza halafu tutachagua,” amesema GK. “Hii ni project ya East Coast. Kuna kwenda nje kufanya video lakini tunataka kwenda speed. Leo tunakaa tena kupanga. Tumeshachukua kabisa nyumba sehemu ya vyumba kadhaa tutakaa mule tutajiandaa. Kuna vitu vingi vitaendelea hapo. Unajua toka East Coast imetoka ilikuwa inafanya muziki fulani tofauti lakini ni Hip Hop, aina fulani hivi ambayo ndio maana umeona watu wameendelea kumiss na wanatuona tunachelewa.”
Wasanii wa East Coast AY, GK, Snare pamoja na Buff G
GK ameimbia Bongo5 kuwa wapo kwenye maandalizi ya mwisho kuingia kambini na kuanza kazi hiyo.
“Tumechagua ma-producer wanne, tumemchagua Marco Chali, tumemchangua John Maundi, Mr T Touch na kuna mwingine mmoja. Producer wote watatengeneza halafu tutachagua,” amesema GK. “Hii ni project ya East Coast. Kuna kwenda nje kufanya video lakini tunataka kwenda speed. Leo tunakaa tena kupanga. Tumeshachukua kabisa nyumba sehemu ya vyumba kadhaa tutakaa mule tutajiandaa. Kuna vitu vingi vitaendelea hapo. Unajua toka East Coast imetoka ilikuwa inafanya muziki fulani tofauti lakini ni Hip Hop, aina fulani hivi ambayo ndio maana umeona watu wameendelea kumiss na wanatuona tunachelewa.”
NAIBU WAZIRI WA AFYA WA ZAMANI LUCY NKYA ADAIWA KURUSHIANA RISASI NA MWANAE, MWANAE AKANUSHA
Dk. Lucy Nkya
|
Kumekuwepo na taarifa kuwa aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa
Afya Dk. Lucy Sawere Nkya na mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki na
mwanae wa kiume Jonas Nkya wamerushiana risasi za moto kwenye ofisi yake mjini
Morogoro kwa kile kilichodaiwa kimetokana na ‘Mzozo wa Kifamilia.’
Hata hivyo akiongea na kituo cha runinga cha ITV jioni hii,
Jonas ambaye ni Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Morogoro,
amekanusha taarifa hizo na kudai kuwa bunduki aliyokuwa nayo ilijipiga
kimakosa.
“Ni uongo tu ndugu mtangazaji ni uongo na sijui imekuwa vipi
mpaka imefika hapo lakini sio kweli,” amesema Nkya. “Ni kitendo tu hiyo risasi
ilivyojifyatua hapo Faraja wala mama mwenyewe hakuwepo ofisini. Sijui hata mama
mwenyewe silaha hana. Kwahiyo hatuwezi kurushiana risasi lakini tatizo ni kwamba
hapa kuna polisi, kuna majirani, kuna nyumba za watu baada ya risasi kujipiga
wakapaniki, sasa sijui kwanini wamefika stage ya kurushiana risasi mimi na mama
yangu, sio ukweli,” ameongeza.
Jonas Nkya
|
“Nilikuwa naye pamoja tumeamka pamoja na mimi nimemuaga
amekwenda kwenye shughuli zake mimi nimeenda kubadilisha gari niende shamba,
tuna utaratibu kila Jumamosi ninaenda shamba kwahiyo hicho ndicho kilichotokea
hakuna! Hata mimi nimeanza kupata hizi habari nipo shamba nimerudi hapa
nakutana na waandishi wa habari tena barabarani, hakuna kitu kama hicho.”
Akizungumzia jinsi risasi ilivyofyatuka alisema:
“Kwanza ni kitu ambacho kimenishitua, kwanini wamemuingiza
mama kwenye suala kama hilo? Kwa sababu ilikuwa ni nje na mama alikuwa hayupo,
yupo ndani ofisini kwake, sasa kama tungerushiana risasi ingekuwa ofisini
kwake! haikuwa hivyo. Hii silaha inakaa kiunoni na mimi natoka kwenye gari dogo
naingia kwenye gari na ikaanguka kupitia mguu wangu wa kulia na risasi yenyewe
ya kizamani ikajipiga risasi moja ambayo ilikuwa kwenye chamber, moja tu! Sasa
baada ya kusikia na wakaona hamna kitu wakaondoka, sasa baadaye huku nyuma ndo
ninaanza kupigiwa masimu kwamba kuna habari kama hiyo, sijui tulikuwa kwenye
kikao, wengine wanasema nilikuwa naumwa malaria sijui! Sielewi kwakweli,
sielewi!”
“Lakini ukweli ndo huu nakwambia, hapo ofisini kulikuwa kuna
mlinzi, hapo ofisini kuna wafanyakazi leo jJmamosi kulikuwa hakuna watu wengi,
halafu nilikuwa na dereva wangu pia, mwana James alikuwa yupo, wanamfahamu na
nimeshawaambia wanaweza kumuuliza! Pia nimewaambia wakamtafute mama, sema mama
mwenyewe yupo na kazi zake kwahiyo nimewaomba ili kupata vizuri ukweli
wakamuone atawaeleza, hakuna habari kama hiyo,” alisisitiza Jonas.
Jonas amekanusha uvumi kuwa yeye na mama yake hawaelewani.
“Hapana hapana mimi na mama yangu nipo naye vizuri, tunaishi
pamoja kwa sababu ya kumsaidia baba yetu. Leo asubuhi tumeamka naye, tumeongea,
tumeagana, yeye anakwenda na shughuli zake mimi nakwenda shamba tumetoka nyumba
moja! Kwahiyo kama ugomvi ungefanyika nyumbani sio ofisini. Kwahiyo nataka
kusema ukweli hizo taarifa hakuna ukweli hata kidogo.
Jonas amewaasa wananchi kutoamini kwa haraka habari
wanazozisoma mtandaoni bila kufanya uchunguzi.
“Cha kwanza nataka kuwaambia ni uongo, lakini pia naomba
jamani hao wenzetu wawe makini na social media. Kwanza wawe wakweli na cha
msingi tusichafuane kabisa. Kama kuna mambo ya siasa haina haja, tusichafuane
kiasi hicho! Obvious jiulize kwanini mama hakuwepo, halafu wanasema nilikuwa
nataka kumpiga mama yangu,” alihoji.
Hakuna taarifa hadi sasa iliyotolewa na Mama Lucy Nkya.
Chidi Benz akamatwa na dawa za kulevya airport
Chidi Benz amekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa anaelekea jijini
Mbeya kwenye show ya Instagram Party inayotarajiwa kufanyika kesho.
Akizungumza Bongo5 leo msanii Shetta ambaye alikuwa naye pamoja
katika safari hiyo ya kuelekea Mbaya, amethibitisha kukamatwa na kwa
Chidi akiwa na vitu vinavyohisiwa ni madawa ya kulevya.
“Kweli tulipata matatizo na Chidi pale airport ila mimi nikaruhusiwa
yeye nikamuacha, amekamatwa na mambo mambo fulani sema ongea na wahusika
watakwambia zaidi,” alisema Shetta.
Akizungumza na Millard Ayo, kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi
Selemani kamanda wa polisi katika uwanja wa ndege Dar es Salaam amesema
Chidi Benz amekiri kuwa dawa hizo ni zake.
Amedai kuwa Chidi alikutwa na kete 14 za dawa za kulevya pamoja na misokoto miwili ya bangi iliyokuwa mifukoni mwake.
Chidi atapandishwa mahakamani hivi karibuni kwa kosa la kukutwa na dawa hizo.Polisi wa uwanja wa ndege tayari wameshathibitisha tukio hilo la kumkamata msanii huyo.
Hii ndio historia ya mziki ya mareheme YP kutoka TMK Wanaume Family
YP, CHEGE NA TEMBA |
Wiki hii hapa tasnia ya bongofleva ilimpoteza msanii maarufu YP
pichani ambaye anaunda kundi la TMK Wanaume Family.Msanii huyo ambaye
jina lake halisi ni Yessaya Ambikile alifariki usiku wakuamkia Jumanne
katika hospitali ya Temeke.
Said Fella ambaye ni meneja wa kundi hilo amesema kuwa marehemu
alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kifua kwa muda mrefu na ndo kitu
ambacho kimechukua uhai wake.
Historia yake katika muziki:
Saidi Fella anasema kuwa alikutana na marehemu YP kwa mara ya
kwanza mwaka 2004 katika ukumbi wa King Palace huko Temeke.Baadae
kulikuwa na shoo ya TMK Wanaume Family katika ukumbi wa Luxury Pub
marehemu akamfata akaomba amsaidie kimziki, ndipo Fella akamwambia
amwimbie, akamwimbia wimbo wake uliokuwa unaitwa ‘Saidali’ na huo ndo
ukawa mwanzo wakuitwa kwenye kundi hilo.
Alivyofika kwenye kundi baada ya kumwambia Juma Nature kuhusu
kipaji cha marehemu, Nature akamwambia kama yeye Fella ameona marehemu
ana uwezo basi ni sawa apewe nafasi katika kundi hilo.
Mwaka 2005 marehemu pamoja na msanii mwingine wa kundi hilo Y Dash
akatoa wimbo wao wa kwanza ‘Shemsa’ ambao ulifanya vizuri na
kumtambulisha msanii huyo kwenye tasnia ya muziki.Kutokana na sauti ya
marehemu kuendana na msanii mwenzake Y Dash wakatoa wimbo mwingine
uliokuwa unaenda kwa jina la ‘Pumzika’.Said Fella aliendelea kueleza
kuwa marehemu alitoa wimbo ulioenda kwa jina la ‘Mapengo matatu’ ambao
ni wimbo alioimba kutokana na kufiwa na baba yake,mama yake na mdogo
wake.Mwaka 2006 marehemu pamoja na Y Dash ambaye kwasasa yuko nchini
Afrika Kusini wakatoa album ya pamoja waliyoipa jina la ‘Mapengo
matatu’.
Baada ya hapo marehemu akaendelea kushiriki kwenye kazi zingine za
wasanii wa kundi la Tmk Wanaume Family na kazi za kundi kama ‘Twende
zetu’ , ‘Dar mpaka Moro’, ‘Kichwa kinauma’ na nyingine nyingi.
Mwaka 2008 marehemu aliamua kuondoka katika kundi hilo na msanii
mwenzake Y Dash pamoja na Jebby wakaenda kundi lingine ambalo walilipa
jina la TMK Unity.Said Fella anasema mwaka 2010 msanii huyo alimtafuta
nakumuomba kurudi katika nafasi yake tena ndipo alipomkubalia nakuwa
kwenye kundi hilo mpaka kifo chake.Baada yakurudi TMK Wanaume Family
nyimbo ambazo alizoshiriki marehemu nakufanya vizuri ni ‘Kichwa
kinauma’, ‘Tunafurahi’ ya Mh Temba na Chegge.
Meneja huyo wa kundi hilo anasema kuwa kundi hilo limepata pengo
kwasababu toka mwanzo kabla wakati TMK Wanaume Family kuvunjika msanii
huyo alikuwa ni kati ya wale wasanii 11 wa mwanzo.Said Fella alifanunua
kuwa alikuwa akianza Juma Nature,Chegge,Kr,Mh Temba na wengine na yeye
YP anakuwa na namba.Kitu kingine alisema kuwa watamkumbuka YP kwa
ucheshi na ubunifu wa staili za kucheza. “Yaani zile staili zote za TMK
Wanaume Family kama mapangashaa nyingi alikuwa akizibuni marehemu pamoja
na Kr, alikuwa ni mtu anayependa kucheza, mtu wakutengeza step”, Said
Fella.Alieleza kuwa kazi ya mwisho ya kundi marehemu kurekodi ilikuwa ni
mwezi uliopita katika studio za Sound Crafters.
Pia msanii wa kundi hilo Chegge alimzungumzia marehemu nakusema kuwa
alipatwa na uchungu hadi anajikuta analia kwasababu watu wengi walikuwa
wakizifananisha sauti zao na ndo maana alipenda kumshirikisha kwenye
nyimbo zake.Msanii mwingine wa kundi hilo Mh Temba alisema kuwa
atakumbuka ucheshi wa marehemu na pia ubunifu wake katika kutunga
viiitikio(chorus) za nyimbo. “Kwakweli TMK Waunaume Family tumepoteza
jembe.
Marehemu Yessaya Ambikile alizikwa jana katika makaburi ya
Chang’ombe Maduka mawili alizaliwa tarehe 10 November mwaka 1986 jijini
Dar es salaam akiwa ni mtoto wa kwanza, kisha akapata elimu ya msingi
katika shule ya msingi Keko Magurumbasi.Baada yakumaliza elimu ya msingi
marehemu hakuendelea na masomo akaanza kujishughulisha na muziki mpaka
kifo chake.Marehemu ameacha mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 8
pamoja na mzazi mwenzake ambaye alikuwa ana mpango wakufunga ndoa
hivikaribuni.
Mungu ampuzimshe kwa amani YP.
IPHONE 6 NA 6 PLUS MILIONI 10 ZIMESHANUNULIWA HADI SASA!
Kampuni ya Apple imedai kuwa hadi sasa imeshauza simu zake
mpya za iPhone 6 na iPhone 6 Plus milioni 10 ikiwa ni siku tatu tu tangu
ziingie sokoni.
Hadi sasa iPhone hizo mpya zipo Marekani, Australia, Canada,
Ufaransa, Ujerumani, Hong Kong, Japan, Puerto Rico, Singapore na Uingereza.
September 26 zitafika kwenye nchi zingine 20 na zingine zilizosalia mwishoni
mwa mwaka huu.
CEO wa kampuni hiyo, Tim Cook Jumatatu hii alidai kuwa
mahitaji ya simu hizo yamezidi matarajio yao.