Baada ya kifo cha Goldie siku chache zilizopita, msanii
mashuhuri na mkongwe katika tasnia ya filamu nchini Nigeria Justus Esiri amefariki
dunia akiwa na umri wa miaka 70. Kutokana na taarifa kutoka vyombo mbalimbali
nchini humo muigizaji huyo ambaye ni baba mzazi wa msanii maarufu wa muziki Dr.
Sid amefariki dunia jumane tarehe 19, 2013.