KWANINI HUKUITWA BAADA YA USAILI? YAJUE MAKOSA YANAYOFANYWA KWENYE USAILI
Kama huna mtu unayemfahamu kwenye taasisi au kampuni
uliyoomba kazi, ni vigumu kujua kwanini hujaitwa baada ya usaili. Hivyo kuna
baadhi ya mambo ambayo yatakufanya usiitwe, na haya ni mojawapo;
1 1. Makosa katika CV
yako
Hiki ndicho kitu cha kwanza kwenye
orodha ya mambo yanayowaangusha wengi. Wakati unaandiaka CV yako au barua ya
kuomba kazi hakikisha tena na tena kama ulichoandika ni sahihi na hakuna makosa
ndani yake. Vile vile unaweza kumpa mtu mwingine aiangalie kabla hujaituma, ili
kukusaidia kuangalia makosa ambayo labda wewe hujaweza kuyaona. Hakuna mwajiri
ambaye anataka kuchukua jukumu la kurekebisha makosa uliyofanya wakati wa
kuandika.
2. Kutokuwa na ujuzi mzuri wa Usaili
Katika usaili wowote, kama ni ana kwa ana au kwenye simu
kujua kuongea lugha vizuri na matamshi yake ni jambo la muhimu sana.Lugha za
mtaani na vifupisho vya maneno vinawezekana katika maisha ya kawaida na
inakubalika kwa jamii ya watu wanaokuzunguka lakini hayaleti picha nzuri kwa
mwajiri hasa unapoyatumia kwenye Usaili. Hakikisa siku ya kwenda kwenye Usaili
, ulale vizuri na kama ni mtu wa kwenda kwenye starehe siku hiyo upunguze kwani
mtu ni rahisi kukugundua kama ulichelewa kulala.
2. 3.
Jumbe zisizoeleweka kwenye mitandao ya Jamii
Hili ni jambo la kizamani, lakini
lisikushangaze. Uwe makini kwenye mitandao ya jamii wewe unaweka vitu gani,
jumbe gani. Kama wakati wote unaonesha picha za wewe ukistarehe, kunywa pombe
na tabia zingine za ajabu ajabu unapoomba kazi zafisha anuani zako za mitandao
ya kijamii kabla ya kuomba kazi.
4. Kutokuonekana kwenye Mtandao
Hii haimaanishi ni kigezo cha kila kazi, ni baadhi ya kazi
tu. Ila kama unatafuta kazi kwenye Masoko, Uhusiano na jamii, Matangazo
,burudani na Nyanja zingize za habari waajiri wengi wanapenda kuona mtu ambaye
ana taswira nzuri na yenye nguvu kwenye mitandao. Kama haujui kitu gani
kinaendelea kwenye teknolojia ya habari tafsiri yake ni kwamba uko nyuma sana
katika kujua mambo yanavyotakiwa kwenda.
5. Kuwa mfuatiliaji Sana
Watu wengi hufikiri kwamba waajiri wanafanya kazi ya
kuwatafutia wao kazi. Ukweli ni kwamba taasisi zote za kuajiri zinataka kujaza
nafasi za kazi zilizowazi kwa wateja wao. Na wanashughulikia wateja wengi kwa
wakati mmoja na kujaza nafasi nyingi kwa wakati mmoja. Kwahiyo kumtumia mwajiri
email au kumpigia simu yule amabye hakukujibu usifikirie kuwa utaonekana kwamba
unastahiki ya kazi, ila watakuona unawachosha hivyo hawatahitaji kushughulika
na wewe.
6. Wewe si Mvumilivu Sana
Kwa upande mwingine, kuna waajiri wengine watakupigia kupata
habari zaidi kuhusu wewe, hakikisha unajibu kwa haraka na ufasaha wakati wote
unapopigiwa simu. Kama kila wakati mwajiri anakupigia na kukufuatilia sana
kuhusu habari zako inamaanisha hujamshawishi vyakutosha kwa kazi ile uliyoomba
na vinginevyo inaweza kuwa sahihi.
7. Umekuwa Ukijilinda ili watu wasiwasiliane na wewe.
Kila mwajiri anakutana na jambo hili. Mtu anaweka tangazo la
kutafuta kazi kwenye tovuti na anasahau kwamba litakuwepo hata baada ya kupata
kazi. Kama hujawahi kuwa na anwani kwenye linkedin au mtandao mwingine
usifikiri ni rahisi mtu kuwasiliana na wewe kuhusu kazi. Hata kama hupendi kazi
iliyotangazwa, usiondoe anwani yako au CVhuwezi jua kwamba utapata fulsa
nyingine.
8. Huna vigezo vya kupata kazi hiyo
Wakati umekata tamaa unafanya maamuzi ya kukatisha tamaa.
Hata kama huna kazi na huna hela ya kutosha , hivyo unaomba kazi sehemu nyingi
hata kama vigezo vyako havikubaliki haitakusaidia na hutapata nafasi ya
kuajiriwa. Kama kitu ambacho mwajiri atakujua kwa sababu mbaya ni wewe siku
zote kutokuwa na vigezo vya kazi.
Unapotafuta kazi hasa kwa makampuni yanayoajiri inabidi uwe
mkweli, nenda na wakati na mwenye maelezo ya kutosha, kwakuwa mwajiri ni daraja
la wewe kutokuajiriwa au kufanikiwa kitaaluma.
0 comments: