Home » Posts filed under Enterteinment
Showing posts with label Enterteinment. Show all posts
Showing posts with label Enterteinment. Show all posts
P-Square waondokewa na baba yao mzazi Mr. Okoye
Miaka miwili baada ya kumpoteza mama yao mzazi, mapacha wa
kundi la P-Square la Nigeria Peter na Paul pamoja na kaka yao Jude Okoye
wamepatwa na msiba mwingine. Wameondokewa na baba yao Mr Okoye aliyefariki
dunia Jumatatu Nov.24.
Vyanzo vya karibu vimesema kuwa Mr. Okoye alidondoka akiwa
anaelekea hospitali huko jijini Lagos. Inadaiwa kuwa siku chache kabla
hajapatwa mauti alifanyiwa upasuaji wa goti na alikuwa akiendelea vizuri.
Diamond kuiachia ‘Ntampata Wapi’ kesho
Diamond Platnumz anatarajia kuachia wimbo wake mpya ‘Ntampata Wapi’ kesho. Wimbo huo ambao huenda ukawa ndio ule aliouonjesha hivi karibuni, utakuwa ni mpya tangu Bum Bum na Mdogo.
Swali ni je! Ataweza kuvunja rekodi ya Mwana FA na Alikiba ya wimbo uliosikilizwa na kupakuliwa zaidi kwenye mtandao wa Mkito?
Sitti Mtemvu bado kiti cha moto, mamlaka zajipanga kumpeleka mahakamani
Uamuzi mgumu wa kujivua taji la Miss Tanzania 2014,
haujamaliza misukosuko inayomkabili Sitti Mtemvu. Wakala wa Uzazi, Vifo na
Ufilisi (Rita) wamedai kuwa wamekamilisha upekuzi wa taarifa alizotumia kuombea
cheti cha kuzaliwa na vielelezo hivyo vimepelekwa polisi.
Ofisa mtendaji mkuu wa Rita, Phillip Saliboko na Meneja
masoko na mawasiliano, Josephat Kimaro wameliambia gazeti la Mwanachi kuwa
upekuzi wa nyaraka zilizotumiwa na Sitti uliofanywa na wanasheria wao, tayari
umekamilika.
“Kazi yetu (Rita) tumeimaliza na upekuzi wa taarifa za Sitti
umekamilika na kinachofuata sasa ni kupeleka nyaraka hizo kwenye mamlaka
inayohusika ambayo ni polisi, wao ndio wataamua nini cha kufanya,” Kimaro
aliliambia gazeti hilo.
Alisema Rita haiwezi kumhukumu moja kwa moja mrembo huyo
kuwa alighushi nyaraka na kudanganya ili apate cheti hicho cha kuzaliwa
kilichotolewa na Rita Septemba na badala yake wanapeleka vielelezo walivyonavyo
polisi ili nao wavifanyie kazi.
“Sisi (Rita) jukumu letu lilikuwa ni upekuzi wa nyaraka,
kazi ambayo imefanywa kwa ustadi mkubwa na jopo la wanasheria wetu na hadi sasa
imekamilika na kinachofuata ni kuzipeleka nyaraka hizo polisi ambao wao ndiyo
wenye jukumu la uchunguzi na kumchukulia hatua Sitti au la,” alisema.
Sitti Mtemvu aliingia kwenye kashfa ya kudanganya umri wake
na nyaraka zake mbalimbali zilionyesha alizaliwa 1989, umri ambao umepitiliza
ule unaotakiwa kwa mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania, huku cheti chake
kikionyesha alizaliwa 1991, hivyo kulazimika kuvua taji hilo.
Source: Mwananchi
Jose Chameleone: Sijamuomba collabo Diamond, mimi si msanii mchanga
Msanii mkongwe wa Uganda, Jose Chameleone, amekanusha ripoti
zilizoandikwa kwenye mtandao wa BigEye wa Uganda kuwa amemuomba Diamond
Platnumz wafanye collabo.
Chameleone ameiambia Bongo5 kuwa application ya Mziiki
ambayo Diamond ni balozi wake wa Tanzania ipo kwenye mazungumzo naye ili
kumfanya balozi wake wa Uganda na hivyo ilimuomba afanye wimbo na Diamond kama
anthem ya Afrika Mashariki.
“Lakini we talked about business na hatujamalizana nao.
Lakini sio eti mimi nimempigia (Diamond) kumuomba tufanye collabo na kitu kama
hicho,” amesema Chameleone. “Wale wa Mziiki app ndo wanahitaji mimi na yeye
tufanye kazi ya anthem ya Mziiki app. Wanajaribu kuunganisha yeye na mimi
tufanye collaboration lakini sio eti mimi nimemuwhatsapp na nimemuomba
collaboration , that’s not right,” amesisitiza hitmaker huyo wa Valu Valu.
“Am not at a level of asking for a collaboration from any artist
in that manner. Sio kwamba sina heshima yake (Diamond) au kitu kama hicho
lakini that’s not the truth, haiwezi kuwa hivyo. I have been doing music for
the past 14 years, right? So I am not an upcoming artist.”
Msikilize zaidi hapo chini.
CHIDI BENZ ASIMULIA STORY NZIMA JINSI ILIVYOKUWA HADI KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA AIRPORT
Rashid Makwiro a.k.a Chidi Benz ambaye ameachiliwa kwa
dhamana Jumatano wiki hii, amesimulia jinsi ilivyokuwa hadi kukamatwa Ijumaa
iliyopita Oct.24 na dawa za kulevya kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Julius
Nyerere.
Chidi alizungumza na Soudy Brown kupitia So So Fresh ya
Clouds FM jana.
“Sikuwaambia natumia, niliwaambia dawa ambazo nilikuwa niko
nazo lazima nitakuwa nimeconfuse kipindi ambacho natumia nilikuwa ofcoz naweka
weka naficha ficha kwenye nguo nguo zangu na nini, so nimewambia maybe
kwasababu hiyo nguo sijawahi vaa ndio mara ya kwanza…huwa naweka mashati kadhaa
nayatundika tu hivi yako kama kumi kumi na tano, huwa nikivaa najua hili
nasafiri nalo au nazunguka tu leo round za town baadae nikilivua nalitupa tu si
unajua sisi mara nyingi nguo ukivaa unakuwa unavaa mara moja labda hivyo. So
nahisi lazima ile dawa nilikuwa nimeiweka labda niliiweka au nimeficha coz
nilikuwa naweza nikachukua hivi enzi zile sitaki mtu aone na nini naiweka
kwenye mfuko naiacha hapo na hilo shati sijawahi vaa ndo nimelivaa juzi. “
alisema Chidi Benz.
“Shetta alinipigia simu akaniambia tunaondoka leo
nikamwambia ooh yeah? Ooh yeah leo fasta, na mimi sasa hivi nakaa Tegeta
unajua, so nikachukua lile shati fasta sio la kupiga pasi ni kama hili
nililovaa hapa nikalichukua tu nikalipiga na jeans hivyo. Nikaenda zangu
airport, niko airport nikamwambia Shetta namtania tu hivyo namwambia mdogo
wangu nimebeba mambo nimebeba mambo [kicheko], nimebeba mambo kibao yale mabegi
yamejaa yote haya yote mabegi sina nguo wala viatu wala nini hapa nina mambo tu
like namtania unajua, lakini sasa nafika pale nasachiwa ndo nakutana na hiyo
dawa”.
Aliendelea,
“Imagine nimekutwa na dawa kwenye mfuko wa shati kushoto
unajua si kama nimeficha au nimefanya nini. Of course kila mtu anaongea cha
kwake hamna yule muongo atakuwa hivi hamna mteja yule of course, so saivi
lazima nikubali kwa kila mtu anachokiongea as long kwamba watu walikuwa
hawasaidii chochote time ambayo sijakamatwa au sijakutwa hamna kitu chochote
walikuwa mtu nasaidiwa au naambiwa kwahiyo naona kawaida tu.
Lakini si kitu nimepanga si kitu nilikuwa nimeplan unajua
nimekutwa nayo mimi mwenyewe ndio nimejisachi, si yeye sijakamatwa mimi
mwenyewe nimejisachi nimezitoa kushoto kulikuwa na pesa kulia pesa kushoto pesa
tena akaniambia we pesa pesa akaniambia hapa mfukoni juu kuna nini, nikamwambia
hii I think ni uchafu uchafu tu natoa hivi nakuta vidude kama kadhaa hivi
naviona tu mkononi hapa, jamaa akaviona akaniambia bwana hii nini nikamwambia
hii…dawa but sijui imekuaje na mimi pale kidogo kibinaadam nilikuwa kama kidogo
akili imeniruka kuja kugundua kwamba ile ni dawa na nimeitoa mwenyewe unajua…
Yaani kwanza nakwambia kwasababu hata yeye wakati natoa hizo
pesa nilikuwa kama namtania yule jamaa ananiambia mfuko wa nyuma namwambia hizi
pesa huku pesa, hii karatasi yangu ya mashairi nataka niandike, hii huku pesa
akaniambia na hapa juu nikamwambia hapo juu hamna kitu ni uchafu uchafu tu, hee
natoa hivi nakutana na kimkanda unajua so like kama nilipigwa na butwaa hivi
unajua.”
Chidi alisema
alijaribu kuwaomba wana usalama wamuelewe na kumsamehe lakini ilishindikana.
“Nikajaribu kuwaomba jamaa nikawaambia bwana sorry kuna time
nilikuwa natumia hizi vitu but nikaachana nazo, so wakati naachana nazo ofcoz
zamani nilikuwa sio mtu wa kununua kimoja kimoja nilikuwa nanunua labda kadhaa
unajua so navyohisi labda siku nilizichomeka kwenye kamfuko haka ka juu wa shati
nikaziweka hapa nimesahau nguo nimeivaa tu ghafla nimesahau kiukweli, so please
kama mnaweza kunielewa mkanisamehe please, hakuna ninachosafirisha hakuna nini
mabegi yangu haya hapa mnaweza mkanisachi nisachini kote, wakasachi kila begi
kila kitu hakuna kitu sina kitu kingine, nilikuwa na spika nilikuwa na viatu
nilikuwa na nguo done.” alimaliza Chidi Benz
Kesi yake imepangwa kusikilizwa tena November 11.