Chidi Benz akamatwa na dawa za kulevya airport
Chidi Benz amekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa anaelekea jijini
Mbeya kwenye show ya Instagram Party inayotarajiwa kufanyika kesho.
Akizungumza Bongo5 leo msanii Shetta ambaye alikuwa naye pamoja
katika safari hiyo ya kuelekea Mbaya, amethibitisha kukamatwa na kwa
Chidi akiwa na vitu vinavyohisiwa ni madawa ya kulevya.
“Kweli tulipata matatizo na Chidi pale airport ila mimi nikaruhusiwa
yeye nikamuacha, amekamatwa na mambo mambo fulani sema ongea na wahusika
watakwambia zaidi,” alisema Shetta.
Akizungumza na Millard Ayo, kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi
Selemani kamanda wa polisi katika uwanja wa ndege Dar es Salaam amesema
Chidi Benz amekiri kuwa dawa hizo ni zake.
Amedai kuwa Chidi alikutwa na kete 14 za dawa za kulevya pamoja na misokoto miwili ya bangi iliyokuwa mifukoni mwake.
Chidi atapandishwa mahakamani hivi karibuni kwa kosa la kukutwa na dawa hizo.Polisi wa uwanja wa ndege tayari wameshathibitisha tukio hilo la kumkamata msanii huyo.
0 comments: