Rapper Navio ambaye yupo Bongo asema anatamani kufanya collabo na Izzo Bizness


Humbled…Hii kubwa sana kwangu”, ni maneno aliyoyasema rapper Izzo Bizness kuelezea furaha yake baada ya kumsikia rapper mkubwa wa Uganda Navio akimtaja kwenye radio kuwa angependa kufanya naye collabo.

 Navio yupo Tanzania, na jana (Nov.18) alifanyiwa mahojiano kwenye kipindi cha Power Jams kupitia East Africa Radio. Alipoulizwa wasanii wa Bongo ambao anatamani kufanya nao collabo, miongoni mwao alimtaja rapper Izzo Bizness.


  Izzo alipost tweet yake Instagram na kuandika “Hii kubwa sana kwangu big up kwa #NAVIO #HAINAKUFELI”

Izzo amezungumza na Bongo 5 kuhusu mpango wa kufanya collabo na Navio kabla hajaondoka nchini.

“Yeah plan zipo tunataka kufanya ngoma, tulikuwa turekodi jana lakini kutokana na ratiba yake ilivyokuwa tight kwaajili ya interviews na nini mpaka muda aliofika alikuwa tayari kaishachoka tayari kwahiyo akaona tuisogeze mbele, tujaribu kuwasiliana leo mapema halafu tujue tunafanyaje, lakini mipango ambayo ipo inabidi tufanye ngoma.”

0 comments:

Post a Comment

Recent Posts