IPHONE 6 NA 6 PLUS MILIONI 10 ZIMESHANUNULIWA HADI SASA!
Kampuni ya Apple imedai kuwa hadi sasa imeshauza simu zake
mpya za iPhone 6 na iPhone 6 Plus milioni 10 ikiwa ni siku tatu tu tangu
ziingie sokoni.
Hadi sasa iPhone hizo mpya zipo Marekani, Australia, Canada,
Ufaransa, Ujerumani, Hong Kong, Japan, Puerto Rico, Singapore na Uingereza.
September 26 zitafika kwenye nchi zingine 20 na zingine zilizosalia mwishoni
mwa mwaka huu.
CEO wa kampuni hiyo, Tim Cook Jumatatu hii alidai kuwa
mahitaji ya simu hizo yamezidi matarajio yao.
0 comments: