Jose Chameleone: Sijamuomba collabo Diamond, mimi si msanii mchanga
Msanii mkongwe wa Uganda, Jose Chameleone, amekanusha ripoti
zilizoandikwa kwenye mtandao wa BigEye wa Uganda kuwa amemuomba Diamond
Platnumz wafanye collabo.
Chameleone ameiambia Bongo5 kuwa application ya Mziiki
ambayo Diamond ni balozi wake wa Tanzania ipo kwenye mazungumzo naye ili
kumfanya balozi wake wa Uganda na hivyo ilimuomba afanye wimbo na Diamond kama
anthem ya Afrika Mashariki.
“Lakini we talked about business na hatujamalizana nao.
Lakini sio eti mimi nimempigia (Diamond) kumuomba tufanye collabo na kitu kama
hicho,” amesema Chameleone. “Wale wa Mziiki app ndo wanahitaji mimi na yeye
tufanye kazi ya anthem ya Mziiki app. Wanajaribu kuunganisha yeye na mimi
tufanye collaboration lakini sio eti mimi nimemuwhatsapp na nimemuomba
collaboration , that’s not right,” amesisitiza hitmaker huyo wa Valu Valu.
“Am not at a level of asking for a collaboration from any artist
in that manner. Sio kwamba sina heshima yake (Diamond) au kitu kama hicho
lakini that’s not the truth, haiwezi kuwa hivyo. I have been doing music for
the past 14 years, right? So I am not an upcoming artist.”
Msikilize zaidi hapo chini.
0 comments: