Sitti Mtemvu bado kiti cha moto, mamlaka zajipanga kumpeleka mahakamani
Uamuzi mgumu wa kujivua taji la Miss Tanzania 2014,
haujamaliza misukosuko inayomkabili Sitti Mtemvu. Wakala wa Uzazi, Vifo na
Ufilisi (Rita) wamedai kuwa wamekamilisha upekuzi wa taarifa alizotumia kuombea
cheti cha kuzaliwa na vielelezo hivyo vimepelekwa polisi.
Ofisa mtendaji mkuu wa Rita, Phillip Saliboko na Meneja
masoko na mawasiliano, Josephat Kimaro wameliambia gazeti la Mwanachi kuwa
upekuzi wa nyaraka zilizotumiwa na Sitti uliofanywa na wanasheria wao, tayari
umekamilika.
“Kazi yetu (Rita) tumeimaliza na upekuzi wa taarifa za Sitti
umekamilika na kinachofuata sasa ni kupeleka nyaraka hizo kwenye mamlaka
inayohusika ambayo ni polisi, wao ndio wataamua nini cha kufanya,” Kimaro
aliliambia gazeti hilo.
Alisema Rita haiwezi kumhukumu moja kwa moja mrembo huyo
kuwa alighushi nyaraka na kudanganya ili apate cheti hicho cha kuzaliwa
kilichotolewa na Rita Septemba na badala yake wanapeleka vielelezo walivyonavyo
polisi ili nao wavifanyie kazi.
“Sisi (Rita) jukumu letu lilikuwa ni upekuzi wa nyaraka,
kazi ambayo imefanywa kwa ustadi mkubwa na jopo la wanasheria wetu na hadi sasa
imekamilika na kinachofuata ni kuzipeleka nyaraka hizo polisi ambao wao ndiyo
wenye jukumu la uchunguzi na kumchukulia hatua Sitti au la,” alisema.
Sitti Mtemvu aliingia kwenye kashfa ya kudanganya umri wake
na nyaraka zake mbalimbali zilionyesha alizaliwa 1989, umri ambao umepitiliza
ule unaotakiwa kwa mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania, huku cheti chake
kikionyesha alizaliwa 1991, hivyo kulazimika kuvua taji hilo.
Source: Mwananchi
You may also Like
Followers
Tags 2
Popular Posts
-
New AUDIO | Geez Mabovu - Story | Download Sikiliza & Download Nyimbo ya Marehemu GEEZ MABOVU akiwa amemshirikisha GALATONE
0 comments: