JE? UNAHISI MPENZI WAKO ANAKUSALITI? ZIJUE SABABU NA TIBA YA USALITI KATIKA MAPENZI


Unahisi mwenzi wako siyo mwaminifu? Kwa jumla ni kwamba, kuna watu wengi wanaoonekana wazi kuwa siyo waaminifu. Wengine ukiambiwa huyu ameoa au kuolewa inakupa wakati mgumu kuamini kwa namna anavyoendelea kufanya mambo ya ngono na watu wengine.
Usaliti ni tabia inayokera mno. Ukisikia mwenzi wako amesaliti, ni wazi hutakuwa na furaha naye; Utajiuliza mengi, hasa kutaka kujua sababu na pengine kujua huyo aliyesaliti naye ana kipi ambacho wewe hauna?
Tendo la kusaliti lina maumivu makali hata kusababisha wengine kuchukua uamuzi mgumu kama kujiua, kutokula na tabia nyingine hatarishi zinazofanana na hizo.
Hata hivyo, siyo sahihi kujiua, wala kujiumiza kwa sababu yoyote ile. Wakati mwingine kuachana na fulani huweza kuwa ni jambo jema ili kumpata mtu anayefaa zaidi.
Maumivu ya usaliti yanamhitaji mtu kuwa mwangalifu, vinginevyo anaweza kuchukua uamuzi usio na maana kwake, wala maisha yake.
Utajisikiaje akiwa na mwingine, au siku akikuletea mtoto wa nje ya ndoa?
Hakuna shaka kwamba tendo hili linaumiza, kwamba uko na mtu halafu anakuja na mtoto kutoka nje ya ndoa, au labda unasikia kwamba ana mwingine. Kwa mtu aliyetenda usaliti, nafsi yake humsuta kwa kujiona ni mkosaji.
Msingi wa kuwa na maisha bora ni kuhakikisha unamfanyia mwenzi wako mambo unayopenda wewe kufanyiwa. Hebu fanya kama vile wewe ni mwenzi wako, jione kama vile unasalitiwa, bila shaka ungeumia. Ikiwa utaumia, kwa nini unamsaliti mwingine?
Ishi hivi
Penda kufanya mazuri, yale ambayo wewe ungependa kufanyiwa na mwenzi wako. Penda kuwa na moyo wa huruma, akili yako ifanye kazi ipasavyo kwa kubuni mambo mazuri ya kufanya kwa mwenzi wako; Ni suala la kuelewa kuwa msingi wa kuwa na uhusiano mzuri ni kujiona kana kwamba wewe ni mwenye deni la kumfanyia mazuri mwenzi wako.
Mambo muhimu ya kuzuia usaliti
Kwa sababu baadhi ya watu wamekuwa wakikubali kuwa na wapenzi wengine kwa shinikizo la kiuchumi, hivyo ni jambo la msingi kwa watu walio kwenye uhusiano kuangalia njia za kuongeza kipato kupitia kazi mbalimbali. Wanandoa wanapaswa kubuni miradi ya kufanya, ili hatimaye suala la kiuchumi lisiwe tatizo.
Iwe ni lazima kwa wanawake na wanaume, wote kuangalia namna ya kufanya ili kujiongezea kipato; lengo liwe ni kujitosheleza kipato. Siyo jambo zuri kumtegemea mtu mmoja katika suala la uchumi kwani anaweza kuugua au labda kuwa na matatizo mengine yoyote ya kazi.
Mwanamke ajiepushe na utegemezi, hii itajenga upendo wenye heshima na itamwongezea mwanamume kutambua umuhimu wa uwepo wa mwanamke katika maisha yake.
Mambo mengine ni maarifa juu ya mapenzi na tendo la ndoa.Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha mwenzi wake anafurahia mapenzi yenu kwa maana ya kujaliana, kushauriana, kusikilizana na kuheshimiana. Katika tendo la ndoa, ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anajua ashughulike vipi ili kutoshelezana.
Muhimu kuzingatia
a) Wanandoa wanapaswa kuandaana kisaikolojia kabla ya tendo, kwa mfano kwa kutumiana meseji hasa kama wapenzi hao wako mbali, kuondoa tofauti zao kwa maana ya migogoro na njia zingine za kufanya wapenzi kufurahiana.
b) Kuzijua sehemu za hisia za mwenzi wako (sehemu za mwanamke zipo 12 na kwa mwanaume zipo 5)
c) Unadhifu na usafi wa mwili ni jambo muhimu sana. Ni muhimu pia kuonyesha ushirikiano Fanya ndoa iwe bora; Wanandoa wanapaswa kuwa marafiki wa karibu. Kama kweli mnataka kuwa na raha katika ndoa, fanyeni kana kwamba ninyi ni marafiki na siyo mabosi kama wanavyofanya baadhi ya watu.
Mfanye mwenzi wako awe mshauri na mfariji wako. Uwe mwenye utu; Uwazi, busara, uvumilivu ukizingatia imani ya dini.

0 comments:

Post a Comment

Recent Posts