Young Killer apanga kurudi shule
Young Killer aka Msodoki ana mpango wa kufuata nyayo za kaka
zake wakiwemo Cpwaa, Noorah na wengine. Rapper huyo na hitmaker wa Dear Gambe,
amesema anatarajia kurudi shule mwakani kwajili ya kujifunza IT baada ya
matokeo mabayaya kidato cha nne mwaka jana kula kwake pia.Young Killer alisema maneno haya mjini Singida ambako yupo
kwenye list ya wasanii
watakaotumbuiza leo, Young Killer amesema katika maisha yake kwa sasa anategemea elimu na muziki ingawa muziki anafanya poa na hivyo anahitaji mwakani kujiunga na chuo ili kupata ujuzi wa masuala ya IT aka Information Technology.

“Mwaka jana nilipiga chini kwaHiyo mwaka huu nafanya mishe za
pesa Halafu mwakani nataka nikapate mafunzo ya taaluma ya IT ili niwe na nguzo
mbili elimu na muziki,” alisema Young Killer.
Rapper huyo mwenye umri mdogo, amesema ingawa kuna changamoto
nyingi katika kugawanya muda wa masomo na wa kazi, atajitaidi kuhakikisha
anapata elimu ili apate misingi miwili kama anavyoihitaji.