Home » Unlabelled » Masanja apost picha akimwombea mgonjwa mbele ya maelfu ya waumini, mashabiki wamuita ‘Mchungaji Msanii’
Masanja apost picha akimwombea mgonjwa mbele ya maelfu ya waumini, mashabiki wamuita ‘Mchungaji Msanii’
Masanja akimwombea muumini |
Safari ya kuelekea kuwa mchungaji na mhubiri mkubwa wa kikristo nchini kwa mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya aka Masanja Mkandamizaji inaonekana kuwa ya milima na mabonde lakini haoneshi dalili za kurudi nyuma. Mtumishi wa Mungu
Emmanuel Mgaya akimuombea mgonjwa LeoJumapili kupitia ukurasa wake wa Facebook, ameweka picha inayomuonesha akiwa mbele ya maelfu ya waumini alipokuwa akihubiri neon la Mungu huku akimuombea mgonjwa aliyekuwa ameanguka chini. “Nimeona Mungu wangu akiponya wagonjwa na kufungua walifungwa na magonjwa sugu. Ni maombi yangu Jumapili ya leo, kila jambo lililokusumbua kwa mda mrefu,iwe ni ugonjwa,shida ya Ndoa,kazI,biashara,masomo,laana,nk,Mungu wangu akuhurumie na upokee uponyaji. Tamka maneno haya kwa imani rafiki yangu, asante Mungu kwa kunihurumia,nimeponywa,” aliandika. Hata hivyo mashabiki wake wamemshambulia huku wengine wakimweka kwenye kundi na manabii wa uongo