Mfanyabiashara Moshi matatani kwa video chafu

Moshi. Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, (jina linahifadhiwa) ameingia katika kashfa nzito baada ya kurekodi mkanda wa video ukimwonyesha akimlawiti mfanyakazi wake wa dukani.
Kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu kimeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu anayepatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mtu mwingine kinyume cha maumbile.
Video za mfanyabiashara huyo ambazo zimekuwa gumzo zimekuwa zikisambazwa kupitia mitandao ya simu hususan Whatsapp na nyingine zikiuzwa katika maduka yaliyopo Stendi Kuu ya Mabasi Moshi.
Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo kijana anayemiliki maduka matatu Stendi Kuu ya Mabasi, alirekodi video hizo kwa siri bila mfanyakazi wake huyo kujua na kuihifadhi kwenye kompyuta.
Haijajulikana ni nani aliyeingia katika kompyuta hiyo na kunakili picha hizo ambazo moja ina sekunde 45 na nyingine inayomuonyesha akimlawiti mfanyakazi wake huyo ikiwa na muda wa dakika nane.
Habari za uhakika zilizopatikana zimelidokeza gazeti hili kuwa kwa sasa mfanyabiashara huyo pamoja na mwanamke huyo wametoroka na hawajulikani walipo baada ya kubaini wanasakwa na polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Robert Boaz alipoulizwa jana alisema ingawa hajaona video hizo, lakini kufanya mapenzi kinyume cha maumbile ni kosa la jinai hivyo watamtafuta mfanyabiashara huyo.
Kamanda Boaz alisema polisi wanamsaka ili ahojiwe kuhusiana na video na vitendo hivyo alivyoiita ni vichafu na kwamba kimsingi anatakiwa kujisalimisha mwenyewe ili kumaliza mambo.
Alitoa wito kwa jamii kufuata maadili ya dini zote ambapo zinawataka binadamu waishi kwa kumtii Mwenyezi Mungu.

Recent Posts