Mtambo wa Dawa za kulevya waingizwa nchini, upo Mbezi Beach!
Wakati matukio ya baadhi ya vigogo na wasanii maarufu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulenya hayajapoa, imebainika kuwa mtambo maalumu wa kuchanganya na kuziongezea thamani dawa hizo upo hapa nchini.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa mtambo huo ambao awali ulikuwa unapatikana Mombasa, Kenya, pekee, unatumika kuchanganya dawa za kulevya na kemikali nyingine ambapo nusu kilo ya heroine huongezwa hadi kufikia kilo mbili.
Uchunguzi unaonyesha kuwa kuwa mtambo huo ulioingizwa mwaka huu na kigogo mmoja wa dawa hizo, upo katika nyumba moja iliyopo eneo la Mbezi Beach.
Mmoja wa watumiaji wa dawa hizo ambaye hakutaka kutajwa gazetini kwa kuhofia usalama wake, alisema mtambo huo umerahisisha upatikanaji wa heroine nchini maarufu ‘white sugar’ kama inavyojulikana mitaani.
“Zamani ‘white sugar’ ikitoka shamba (nchi inakotengenezwa yaani Pakistan na nchi nyingine) ilikuwa inapelekwa Mombasa, Kenya, ambako kuna mtambo wa kuchanganya na dawa nyingine ili iongezeke wingi wake, lakini kazi hiyo inafanyika hapa hapa nchini kwa sasa,” alisema.
Alipoulizwa kuhusu uwepo wa mtambo huo hapa nchini, Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema kuwa kuna taarifa alizonazo ambazo bado anazifanyia kazi.
“Hata kama nikiwa nazo nazifanyia kazi, za kwangu mimi nazifanyia kazi na hata za kwako nazifanyia kazi,” alisema Nzowa.
Hata hivyo, Nzowa akizungumza katika kipindi cha Malumbano ya Hoja kilichorushwa na Televisheni ya ITV juzi, alisema kuwa katika siku za hivi karibuni wafanyabiashara wa heroine wamekuwa wakiingiza nchini malighafi za dawa hizo, tofauti na awali ambapo walikuwa wakiingiza dawa hizo zikiwa tayari kwa matumizi.
Akitoa mfano alisema kuna raia wa kigeni alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, akiwa na malighafi hizo zilizokuwa zikifanana na sukari na kwamba Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Mkemia Mkuu wa Serikali, ndiyo waliobaini kuwa haikuwa sukari kama ilivyodhaniwa.
Alisema kutokana na uhaba wa dawa hizo bei ya kete imepanda ambapo hivi sasa hakuna kete ya gramu 0.11 inayouzwa chini ya Sh 3,000.
Hii ni mara ya pili kubainika kuwepo kwa mtambo wa kutengenezea dawa za kulevya nchini. Miaka ya hivi karibuni jeshi la polisi lilikamata mtambo wa kutengenezea dawa za kulevya katika nyumba moja iliyopo eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa mbali ya kuwepo mtambo huo kuna nyumba tano katika eneo la Tandika jijini Dar es Salaam karibu na soko, ambazo zinatumika kuuza dawa za kulevya huku baadhi ya polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, wakiwalinda wauzaji wake kwa kuwapa taarifa ya mipango inayopangwa na jeshi la kuwatia mbaroni.
Alisema kuna wakati askari huonekana wakirandaranda katika mitaa hiyo, kitu kinachowafanya wakazi wa maeneo hayo kuamini kuwa wamefika kukamata, lakini badala yake huishia kuingia katika nyumba hizo kuchukua hongo na kutoka.
“Hata askari wenyewe wakija kukagua hubaki wakishangaa na kushindwa kuamini kama kweli nyumba waliyoambiwa inauza unga ndiyo hiyo waliyoikagua. Ndiyo ‘madili’ hayo watu wanavyoishi mjini hapa,” alisema.
Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, Engelbert Kiondo alisema hawezi kusema ndiyo au hapana kwa kuwa jambo hilo linahusisha vitendo vya rushwa.
“Kuhusu askari kuwalinda wahalifu siwezi kusema ndiyo au hapana kwa sababu hili ni suala la rushwa,” alisema Kiondo na kuongeza kuwa: “Lakini kuhusu kuwakamata vijana wanaojihusisha na dawa za kulevya hao tunawakamata kila siku, wengi wameshafikishwa mahakamani kesi zao zipo katika hatua tofauti.”
Kwa upande wake Nzowa, alisema kwamba Jumatano wiki hii walifanikiwa kuwakamata watu watatu wakijihusisha na dawa hizo, akiwamo mwanafunzi wa kike na kwamba wote walifikishwa mahakamani.
Taarifa zaidi ziliendelea kueleza kuwa dawa aina ya heroin au ‘white sugar’ ndiyo inayopatikana kwa wingi nchini huku ikifuatiwa na ‘cleck’ inayojulikana mitaani kama ‘pele’ kwa kuwa inatoka nchini Brazil.
“Bei ya unga hutegemea aina na kiwango mteja anachokihitaji kwani kipo kipimo cha Sh 1,000 na Sh 2,000 huku kipimo maarufu kama pointi kikiuzwa kati ya Sh3,000 na Sh3,500. Lakini pele huuzwa bei kubwa zaidi, kwani ukubwa wa punje ya mtama tunanunua kwa Sh10, 000,” alifafanua.
Chanzo: Mtambo dawa za kulevya waingizwa nchini - Kitaifa - mwananchi.co.tz