CHADEMA YATOA NYARAKA ZA SIRI KUMJIBU ZITTO KABWE YAWATAKA MSAJILI WA VYAMA NA CAG WAWAJIBIKE



Hii ni taarifa  ya  Chadema:
Kutokana na taarifa zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu
za Serikali kuwa vyama vya siasa ambavyo vinapata ruzuku kutoka serikalini
havijawasilisha taarifa yake ya mapato na matumizi kwa ajili ya kufanyiwa
ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kipindi cha miaka
minne mfululizo, yaani kuanzia mwaka 2009/2010- 2012/2013.
CHADEMA tunapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo juu ya taarifa hizo;
     i.  Kuwa taarifa hizo sio sahihi na
hazina ukweli kuhusiana na CHADEMA labda kwa vyama vingine, hii ni kutokana na
ukweli kuwa tulishawasilisha taarifa zetu za fedha kwa msajili wa vyama vya
siasa na zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2010/2011, 2011/2012 na hili linathibitishwa
na barua ya msajili wa vyama vya siasa yenye Kumb.Na. CDA.112/123/01a/37,
ya tarehe 04 september 2012. Iliyopelekwa kwa makatibu wakuu wa vyama vyote vya
siasa (nakala imeambatanishwa).
Aidha, hesabu za mwaka wa fedha zilizokaguliwa za 2009/2010,
tuliziwasilisha kwa Msajili wa vyama vya siasa kwa barua yenye Kumb.Na. C/HQ/ADM/MSJ/04/71 ya tarehe
27 Octoba, 2011. (Nakala ya barua imeambatanishwa)
    ii. Kuhusu taarifa ya fedha
iliyokaguliwa kwa mwaka huu wa fedha 2012/2013, bado haijawasilishwa kwenye
ofisi za msajili wa vyama kutokana na barua ya msajili wa vyama vya siasa ya
Novemba 26, 2012 yenye Kumb.Na.DA.112/123/16A/97
ambayo ilikuwa na maelekezo kuhusu ukaguzi wa mahesabu ya vyama vya siasa, iliyokuwa
inajibu barua tuliyomwandikia tukitaka kupata ufafanuzi kuhusu ukaguzi wa
hesabu za chama kutakiwa kufanywa na CAG na alitujibu kuwa “tumefanya mawasiliano na Mkaguzi
na Mdhibiti wa Mahesabu ya Serikali (CAG) kwa ufafanuzi wa jambo hili na
tutawafahamisha ipasavyo kuhusu malipo/gharama mliyotakiwa kulipa katika
ukaguzi wa Mahesabu hayo”; mpaka leo hatujawahi kupata ufafanuzi huo
pamoja na ukweli kuwa tumeshafunga hesabu zetu za mwaka kama chama (barua imeambatanishwa).

    iii. Kuhusu taarifa ya fedha kutoka
nje ya nchi, CHADEMA tumekuwa tukiwasilisha taarifa zetu kila mara tunapopata
fedha kwa ajili ya mafunzo na programu nyingine mbalimbali za chama kama
ambavyo msajili alituandikia barua tarehe 19 Agosti 2013 yenye Kumb. Na.DA.112/123/16a/10 iliyokuwa ni
taarifa ya mapato yatokanayo na michango au misaada toka nje ya nchi, alisema “tunashukuru
kwa taarifa hii ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya vyama vya siasa” (imeambatanishwa
barua husika )
   iv.Kuhusu Taarifa za gharama za
uchaguzi kwa mwaka 2010 , tuliwasilisha taarifa hiyo na Msajili alikiri kuwa ni
vyama viwili tu ndiyo vilikidhi utekelezaji wa sheria ya gharama za uchaguzi
kwa ukaguzi wa marejesho, hii inathibitishwa na barua ya Msajili yenye Kumb.Na. CDB.173/205/01/23 ya tarehe 16
April, 2012. (Nakala imeambatanishwa)
Tunapenda kuwahakikishia watanzania kuwa CHADEMA ndiyo ambayo tulidai CAG awe na mamlaka ya kukagua fedha za
vyama vya siasa ili taarifa zake ziwekwe hadharani na tutaendelea kutoa
ushirikiano kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote, kuhakikisha sheria hii
inatekelezwa ipasavyo kuhakikisha uwazi kwenye mapato na matumizi ya vyama vya
siasa.
Aidha, kama ambavyo siku zote tumesimamia na kusisitiza, tunamtaka CAG
akague fedha zote za vyama na sio ruzuku tu kama ambavyo kamati ya Bunge
inataka iwe.
Imetolewa leo Alhamis,
Oktoba 17, 2013;
……………………….
Antony C. Komu
Katibu wa Baraza la
Wadhamini.



0 comments:

Post a Comment

Recent Posts