WAMBURA RUKSA KUGOMBEA URAIS SIMBA
RASMI Kamati ya rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
imemrejeha Mgombea wa Urais wa Simba SC, Michael Richard Wambura kwenye
mbio za kuwania uongozi wa Wekundu wa Msimbazi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Julius Lugaziya amewaambia Waandishi wa Habari mchana wa leo ofisi za TFF katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kwamba Wambura amerejeshwa baada ya kikao chao kilichodumu kwa siku mbili.
Baada ya mlolongo mrefu tangu juzi Saa 5:00 asubuhi hoteli ya Courtyad, Upanga, Dar es Salaam hadi jioni ya jana, Wajumbe wa Kamati hiyo waliamua kupiga kura kuamua na Wambura akapata kura tatu kati ya tano za kumkubalia aendelee na mbio za Urais Simba SC.
Ikumbukwe Wambura alikata rufaa TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kumuengua katika kinyang’anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC chini ya Mwenyekiti Wakili Dk. Damas Ndumbaro ilimuengua Wambura kwa sababu alikiuka Katiba ya klabu hiyo, TFF na FIFA kwa kuipeleka klabu hiyo mahakamani.

0 comments: