Home
» Habari za Kitaifa
» Video: Flora Mbasha Aelezea Kisa cha Mume wake Mbasha Kumtishia Kumuua, na Tuhuma za Kumbaka Shemeji Yake
Video: Flora Mbasha Aelezea Kisa cha Mume wake Mbasha Kumtishia Kumuua, na Tuhuma za Kumbaka Shemeji Yake
Muimbaji wa Injili Flora Mbasha amefunguka kuhusu kisa cha mume wake,
Emmanuel Mbasha kumtishia kumuua, pamoja na tuhuma za kumbaka shemeji
yake mwenye miaka 17, katika Exclusive Interview aliyofanyiwa na Global
Publishers.
“Yani alikuwa mpaka ananitukana matusi ya nguoni kama mtu ambaye hajaokoka”, amesema Flora. “Nikahisi labda kuna kitu amabcho kimemuingia, nikamwambia Mbasha au umerogwa ndugu yangu we unaongea vitu gani hivyo, akawa analalamika tu basi we ndio umerogwa sio mimi.”
Flora ameendelea kusema,
“Na kabla sijatoka ndani alisema we lazima leo nikufundishe adabu alinishika tu akaniniga yani mpaka akaniachia maalama kwenye shingo yani hivi ninavyozungumza mpaka saizi bado shingo yangu inauma yale maumivu niliyoyapata hiyo siku. Nikamwambia Mbasha Mbasha Mbasha unaniuwa hata kuongea siwezi”.
“Huo usiku sikurudi nyumbani na asubuhi Jumatatu yule binti akapiga simu hakunipigia mimi alimpigia mdogo wangu mwingine akamwambia tu mimi naondoka ilikuwa mida kama saa 12 kasoro akasema mi naondoka mi shemeji ameninyanyasa amenidhalilisha kanifanyia kitendo kibaya sana, sasa akamuuliza amekufanyia nini akawa hawezi kuongea kwenye simu akamshauri tu kwamba usiondoke subiri dada yako atakapokuja kwanza anarudi muda si mrefu…kwasababu Yule binti tulikuwa tunakaa nae nyumbani sasa ni miaka kama mitatu au mine naishi nae pale nyumbani namtunza mimi ni mdogo wangu kwahiyo nilikuwa naishi nae hapo ndani kwahiyo alikuwa kama ni mtoto wa kwangu mimi tulikuwa tunamlea pamoja na mme wangu.” Amesema Florah Mbasha.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
0 comments: