NIKKI WA PILI WA ‘WEUSI’ KUACHIA WIMBO MPYA ‘STAKI KAZI’ WIKI IJAYO
Members wa kampuni ya Weusi hawataki kulala, baada ya
kuachia video ya single yao ‘Gere’ siku chache zilizopita rapper wa kundi hilo
Nikki wa Pili naye anajiandaa kuachia single yake mpya ‘Staki Kazi’
inayotarajiwa kutoka wiki Ijayo 13.05.2014
Single hiyo ambayo Nikki amewashirikisha G-Nako na Ben Pol,
imetayarishwa na producer Nahreel ambaye kwa sasa amehamia katika studio ya
Switch inayomilikiwa na rapper Quick Rocka, hapo mwanzo alikuwa Hometown
Records.
Nikki Wa Pili Jumamosi iliyopita aliondoka na tuzo ya wimbo
bora wa Hip Hop kupitia ‘Nje ya box’ huku Weusi wakiondoka na tuzo ya Kikundi
Bora cha mwaka (Kizazi kipya) katika tuzo za KTMA 2014.
0 comments: