Home
» Enterteinment
» BARACK OBAMA, WINNIE MANDELA, LUPITA NYONG’O NI KATI YA WAALIKWA KATIKA HARUSI YA KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN
BARACK OBAMA, WINNIE MANDELA, LUPITA NYONG’O NI KATI YA WAALIKWA KATIKA HARUSI YA KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN
Kanye West na mchumba wake ambaye pia ni mama wa mwanaye Kim
Kardashian wako katika maandalizi ya harusi yao inatarajiwa kufanyika (May 24)
huko Paris, Ufaransa.
Kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu maandalizi ya harusi
hiyo ikiwa ni pamoja na wageni wanaotarajiwa kupewa mwaliko wa kuhudhuria
harusi hiyo.
Kwa mujibu wa jarida la American Heat, tayari Kanye (36)
amempatia msaidizi wake orodha ya wageni 600 anaotaka kuwaalika katika harusi
yao.
Baadhi ya watu mashuhuri ambao wako katika orodha hiyo ya
wageni 600 ni pamoja na Rais wa Marekani Barack Obama, pamoja na Prince William
na mkewe Catherine wa Uingereza.
Kwa mujibu wa jarida hilo mastaa kutoka Afrika ambao wako
katika orodha ya waalikwa ni pamoja na mke wa zamani wa hayati Nelson Mandela,
Winnie Mandela pamoja na staa aliyeiteka Hollywood kwa sasa Lupita Nyong’o.
Mastaa wengine walioko kwenye orodha hiyo ni Jay Z na
Beyonce, Jamie Foxx, Jared Leto, will.i.am, Chris Martin na Oprah Winfrey,
0 comments: