AMBWENE YESAYA AKA AY ANATARAJIA KUACHIA WIMBO MPYA UITWAO ‘ASANTE’.
Ameiambia Bongo5 kuwa wimbo ni maalum kabisa kwa jinsia
zote, kuudedicate kwa watu wanaowapenda kwa dhati. AY amesema wimbo huo
umetayarishwa na Marco Chali na kwamba utatoka hivi karibuni. AY ambaye pia ni
CEO wa kampuni ya Unity Entertainment amesema kwenye Asante anafikiria
kumshirikisha msanii wa kike asiye na jina ili kumtoa kama alivyofanya kwa
Avril na Vanessa Mdee.
Kwa upande mwingine, akiongelea kauli ya Shaa hivi karibuni
kwenye gazeti la Mwananchi aliyedai kuwa collabo za kimataifa kwa wengi ni za
kulazimisha na hutumia fedha nyingi, AY amesema kila msanii ana mipango yake na
hivyo hawezi kumpinga, japo kwake amedai collabo hizo zimemsaidia kwa kiasi
kikubwa.
Amesema harakati za kutafuta collabo za wasanii wa Afrika
alizianza siku nyingi kitu ambacho wasanii wengi wameanza kukishtukia kwa sasa
na tangu hapo jina lake limeenea barani Afrika kwa kiasi kikubwa.
Ameongea kuwa mara nyingi yeye amekuwa na malengo ya muda
mrefu katika kupata matunda yatokanayo na collabo hizo, hivyo kwa wasanii wengi
walio na malengo ya muda mfupi hushindwa kuyaona matokeo mapema na huku wengi
wakitumia gharama kupata collabo hizo.
Pamoja na wasanii wa Afrika wakiwemo P-Square, J-Martins,
marehemu Goldie, Sauti Sol, Maurice Kirya, Jaguar, Prezzo, Avril, Victoria Kimani
na wengine, AY amewahi kushirikiana na wasanii wakubwa wakiwemo Sean Kingstone,
Romea, Lamyia Good, Miss Triniti.
Mwaka jana alitajwa kuwania tuzo mbili za Channel O kwa
video ya wimbo wake, Party Zone.
0 comments: