JOH MAKINI NA NIKKI WA PILI KUFANYA VIDEO TATU MWEZI JANUARY 2014
Rappers ndugu wa kampuni ya Weusi Joh Makini na Nikki wa
Pili, mwezi January 2014 wanatarajia kufanya video tatu za nyimbo zao
zilizotoka na hazina video mpaka sasa.
Joh ameiambia Bongo5 kuwa video ya kwanza wanatarajia
kuifanyia jijini Arusha wiki hii na director Nisher, na kuwa wanatarajia kuondoka
kesho (Dec 31) pamoja na G-Nako kuelekea Arusha kwaajili ya kazi hiyo.
Amesema video ya pili ambayo itakuwa ya single yake na Nikki
wa Pili ‘Bei ya Mkaa’ itafanyika Dar es salaam chini ya muongozaji Adam Juma,
katika wiki ya pili au ya tatu ya January.
Makini ameongeza kuwa video ya tatu anayotegemea kuifanya
mwezi January mwakani ni ya single yake ‘Nikumbatie’ ambayo audio ilitengenezwa
na Fundi Samweli. Joh amesema video ya wimbo huo anategemea kuifanya na
director wa nje.
“Sijajua nafanya na nani video ya Nikumbatie lakini nataka
kufanya na director wa nje…naweza kuja au mimi kwenda ila nitajua nikishaamua
ni nani nafanya nae” Alisema mwamba wa Kaskazini.
0 comments: