Home
» Habari za Kitamaifa
» WAZIRI MKUU WA UKRAINE JULIA TYMOSHENKO AANZA MGOMO WA KUTOKULA CHAKULA NCHINI HUMO.
WAZIRI MKUU WA UKRAINE JULIA TYMOSHENKO AANZA MGOMO WA KUTOKULA CHAKULA NCHINI HUMO.
Waziri Mkuu wa zamani wa Ukraine, Julia Tymoshenko. |
KIONGOZI wa upinzani nchini Ukraine, Julia Tymoshenko leo ameanza mgomo wa kula chakula, akiwaunga mkono maelfu ya watu wanaopinga uamuzi wa serikali hiyo kuubatilisha mkataba baina ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya. Tymoshenko, kiongozi mwenza wa muungano uliofanya mapinduzi yaliyopewa jina la chungwa, mwaka 2004, unaounga mkono mataifa ya Magharibi, alitangaza kuanza mgomo huo katika barua yake aliyowaandikia wafuasi wapatao 20,000 jana Jumatatu wanaounga mkono mkataba wa ushirikiano kati ya Ukraine na Umoja wa Ulaya, ambao wanaandamana mjini Kiev kwa siku ya pili mfululizo. Tymoshenko aliyekuwa waziri mkuu wa Ukraine, amesema ataendelea kugoma hadi hapo Rais Viktor Yanukovych atakaposaini mkataba huo kuhusu ushirikiano na biashara huru na Umoja wa Ulaya. Ameongeza kusema kuwa iwapo Yanukovych hatosaini mkataba huo tarehe 29 ya mwezi huu wa Novemba, atolewe katika uongozi wa Ukraine kwa njia ya amani na kikatiba, pamoja na wasaidizi wake wa kisiasa na wala rushwa
Polisi wakipambana na waandamanaji mjini Kiev. |
Rais Viktor Yanukovych na Rais Vladmir Putin. Uamuzi huo umetolewa baada ya bunge kushindwa kwa mara nyingine kuupitisha muswada wa sheria utakaoruhusu kuachiwa huru kwa Tymoshenko, sharti kuu lililotolewa na Umoja wa Ulaya ili nchi hiyo iweze kusaini mkataba huo. Tymoshenko anatumikia kifungo cha miaka saba gerezani baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka. Jana Jumatatu, polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatanya zaidi ya waandamanaji 100,000 wanaoupinga uamuzi huo wa serikali waliokusanyika mjini Kiev. Umati huo wa watu unaelezwa kuwa mkubwa zaidi kutokea tangu mapinduzi ya chungwa na baadae Viktor Yushchenko kutoka muungano unaounga mkono mataifa ya Magharibi, kushinda katika uchaguzi wa urais mwaka 2007. DW
0 comments: