Ufoo Saro, kulia akiwa na Rais Jakaya Kikwete
Mwandishi wa habari wa kutoo cha runinga cha ITV, Ufoo Saro
chumba cha wagonjwa wa dharura cha hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam
baada ya kupigwa risasi na anayedaiwa kuwa mchumba wake.amelazwa kwenye
Katika tukio hilo lililotolea leo asubuhi, mama mzazi wa
Ufoo ameuawa huku mchumba wake huyo naye akijiua kwa kujipiga risasi.
Taarifa zinadai kuwa mtu huyo ambaye amefahamika kwa jina la
Mushi na kwamba alikuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa, alikuwa kwenye
mazungumzo ya kawaida na wawili hao huko Kibamba ambapo walishindwa kuelewana
na ndipo aliwapiga risasi.
Akiongea na waandishi wa habari leo kwenye hospitali ya
Muhimbili, Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi amesema Ufoo
anaendelea vizuri na anaweza kuongea kwa sasa na kwamba ana imani atapona na
kuendelea na kazi kama kawaida.
Sababu za tukio hilo bado hazijafahamika lakini kwa mujibu
wa chanzo kimoja, linaweza kuwa limetokana na ugomvi wa kimapenzi kati yao.
“Alikuwa mume mtarajiwa wa Ufoo ila jamaa alikuwa akifanya
kazi UN nchini Sudan Kusini ingawa kitengo chake bado hakijafahamika ila kwa
habari za mtaani zisizokuwa na uhakika wanasema alikuwa mwanajeshi. Anaitwa
Mushi. Bwana mushi alikuwa na mgogoro na Ufoo mpenzi wake ila mama mkwe akawa
anamtetea Ufoo.
Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Hemed Msangi
alisema Ufoo alipigwa risasi tumboni na begani na madaktari wanahangaika
kuhakikisha wanaokoa maisha yake. Madaktari wameomba apumzike kwa sasa na hivyo
hakuna mwandishi aliyeruhusiwa kuingia ndani wala ndugu zaidi ya Mengi peke
yake.
Inadaiwa kuwa kufuatia tukio hilo polisi wamegawanyika
katika timu tatu ambapo moja ipo Muhimbili, ya pili Kibamba yalipotokea mauaji
na ya tatu inashughulika mtaani kutafuta taarifa muhimu za mauaji.
Source: Jamii Forums, ITV, Michuzi
|
0 comments: