NAY MITEGO AZIDI KUPASUA ANGA LA MZIKI


Msanii mtata wa muziki wa kizazi kipya Nay wa Mitego amefanikiwa kuuutangaza mziki wake ndani na nje ya nchi hii ni baada ya kuchaguliwa katika kinyang’anyiro cha tuzo za mziki nchini Kenya . Nay ameingia katika kategori mbili katika tuzo za Nzumali nchini Kenya, ameingia katika kategori ya msanii bora wa mwaka wa afrika mashariki na msanii bora wa kiume kutoka Tanzania na ‘’hit song’’ mziki gani akishirikiana barabara na diamond
Akizungumza na vyombo vya habari Nay amewashukuru mashabiki wake wa nchini Tanzania na Kenya kwani wao ndio chachu ya yeyekufanikiwa katika mziki.
“Nawashukuru sana mashabiki wangu kwa sapoti yenu bila nyie mimi nisingekuwa hapa. Tuombe mungu tuchukue tuzo zote mbili ili tanzainia ionekane iko katika orodha ya nchi zenye wanamziki bora’’ alisema nay”
Tuzo hizo zitatolewa novemba 23 nchini humo ambapo anatarajia kushiriki huku akiwa na matumaini makubwa ya kuibuka mshindi

0 comments:

Post a Comment

Recent Posts