Bomu lauwa wengi Beledweyne, Somalia
Mshambuliaji wa kujitolea mhanga amejiripua kwenye mkahawa uliojaa watu katika mji wa Beledweyne, katikati mwa Somalia.
Watu kama 16 wameuwawa na zaidi ya 30 kujeruhiwa.Kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Al Shabab, limesema limefanya shambulio hilo.
Serikali ya Somalia, ikisaidiwa na kikosi cha wanajeshi kutoka nchi kadha za Afrika, inapigana na Al Shabab ili kuidhibiti nchi.
Al Shabab imesema iliwalenga wanajeshi kutoka Ethiopia na Djibouti walioko Beledweyne, lakini walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kwamba waliouwawa wengi walikuwa raia.
You may also Like
Followers
Tags 2
Popular Posts
-
He Yide (5) ambaye amepewa jina la utani la Duoduo mkazi wa Nanjing China ameweka rekodi ya kuwa rubani mdogo zaidi duniani na sijui kama ...
-
Je utawezaje kutambua fursa na kuweza kuanzisha biashara katika mazingira yako? Bila shaka hili swali watu wengi wanaotamani kumiliki bias...
0 comments: