"Operesheni hiyo ambayo mtu huyu
aliuawa ilikuwa muhimu kwa serikali. Mtu huyu alikuwa na jukumu kubwa
kwa raia wengi wasio na hatia na kifo chake kitasaidia kurejesha amani,"
alisema waziri huyo kupitia Radio Mogadishu.
Maafisa kutoka serikali ya Somalia
inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa wamemtaja mwanamgambo aliyeuawa
kuwa anayefahamika vyema kwa kutengeneza mabomu ya kuvaa mwilini pamoja
na ya kutengwa ndani ya gari ambayo hutumiwa mara kwa mara na waasi
kuyashambulia maeneo ya serikali. Hapajakuwa na kauli yoyote kutoka kwa
wapiganaji hao.
Shambulizi hilo linakuja wiki chache
baada ya shambulizi kali kufanywa katika jumba la maduka ya Westgate
jijini Nairobi, Kenya, lililodaiwa kufanywa na al-Shabaab ambapo watu 67
waliuawa.
Kisha kikosi maalumu cha jeshi la
wanamaji la Marekani kikafanya shambulizi katika bandari ya kusini ya
Barawe mapema mwezi huu (Oktoba) na kushindwa kufikia lengo lake: ambalo
lilikuwa ni kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa al-Shabaab na Mkenya
mwenye asili ya kisomali kwa jina Abdulkadir Mohammed Abdulkadir, pia
anayefahamika kama Ikrima.
Afisa mmoja wa Marekani ambaye
hakutaka kutajwa jina lake, hajasema sehemu ambayo ndege hiyo isiyoruka
na rubani ilianzia safari yake, lakini jeshi la Marekani huendesha
shughuli zake za ndege hizo kutoka kambi za nchini Djibouti na Arba
Minch kusini mwa Ethiopia.
Wapiganaji wa al-Shabaab wametimuliwa
kutoka miji mikuu ya Somalia, ikiwa ni pamoja na Mogadishu na bandari ya
kusini mwa nchi hiyo Kismayo, kufuatia operesheni ya jeshi la Umoja wa
Afrika linalosimamiwa na Umoja wa Mataifa na ambalo sasa lina wanajeshi
17,700.
Kundi hilo hata hivyo linayadhibiti
maeneo makubwa ya kusini mwa Somalia na katika kipindi cha miezi kadhaa
iliyopita, limekiongeza kiwango cha mashambulizi yake ya kujitoa mhanga.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
KIONGOZI WA NGAZI YA JUU WA AL-SHABAAB AUAWA SOMALIA
Kiongozi wa
ngazi ya juu anayeongoza mashambulizi ya kujitoa mhanga ya kundi la
al-Shabaab lenye mafungamano na al-Qaeda ameuawa katika shambulizi la
ndege isiyoruka na rubani Kusini mwa Somalia
Waziri wa Mambo ya Ndani, Abdikarin Hussein Guled, ameiambia redio ya serikali kuwa idara ya ujasusi ilikuwa ikimfuatilia Ibrahim Ali Abdi, maarufu kama Anta-Anta, kwa muda sasa kabla ya shambulizi hilo kufanywa jana Jumatatu 28.10.2013
Waziri huyo hajasema ni nani aliyefanya shambulizi hilo, lakini afisa mmoja mjini Washington amesema jeshi la Marekani lilifanya shambulizi la ndege isiyoruka na rubani likililenga kundi la al-Shabaab nchini Somalia jana Jumatatu.

0 comments: