Home » Unlabelled » DAVIDO, ALAINE, IYANYA, MOHOMBI, J-MARTINS NA WASANII WA NYUMBANI ZAIDI YA 40 KULISHAMBULISHA JUKWAA LA FIESTA DAR LEO
DAVIDO, ALAINE, IYANYA, MOHOMBI, J-MARTINS NA WASANII WA NYUMBANI ZAIDI YA 40 KULISHAMBULISHA JUKWAA LA FIESTA DAR LEO
Baada ya Serengeti Fiesta 2013 kuzunguka kwenye mikoa zaidi ya 15 nchini, leo safari inahitimishwa kwa show kubwa ya Dar es Salaam.
Jukwaa la Fiesta ya Dar es Salaam, ambalo ni tofauti kabisa
na mengine yote yaliyowahi kufungwa kwenye viwanja vya Leaders miaka iliyopita,
litakuwa mwenyeji wa wanamuziki watano wa kimataifa.
Mrembo na muimbaji wa reggae tamu ya Jamaica yenye ladha ya
R&B, Alaine anatarajiwa kupanda jukwaani kuwaonjesha mashabiki wake live,
hits zake zisizo na idadi. Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari jana,
Alaine ambaye utampenda kwa ucheshi wake alisema amefurahia kuja kupanda kwenye
jukwaa la Fiesta na atawapa mashabiki wake burudani kali.
“Ninafuraha kugawama upendo wangu, muziki wangu na nguvu
yangu, itakuwa kali sana. Na nimefurahi kuwa pamoja na wasanii hawa wenye
vipaji na kujifunza zaidi kuhusu Tanzania na kuhusu muziki wenu,” alisema
Alaine.
Mkali mwingine atakayeleta ladha ya kipekee leo ni Davido,
anayetarajiwa kuwachezesha mashabiki wa Dar mtindo wa uchezaji wa Skelewu huku
Mnaijeria mwenzie, J-Martins ambaye amekuwa mgeni wa mara kwa mara nchini,
akiwapa burudani nyingine.
Wasichana watapagawa zaidi leo kwenye show hiyo pale ambapo
bingwa wa kuvua shati jukwaani, Iyanya wa Nigeria atakuwa akitumbuiza hits zake
na kuwaonesha six pack yake kifuani na mauno ya hatari. Iyanya anatarajia kutua
usiku wa leo nchini na ataunganisha moja kwa moja Leaders kwenda kutumbuiza.
Burudani haitaishia hapo, mkali mwenye asili ya DRC na
Sweden na msanii wa YMCMB, Mohombi atawasafirisha wapenzi wa burudani kwa
‘safari yenye bumps’ kwa Bumby Ride na kuonesha mapenzi chini ya mti wa mnazi.
Hakuna kusahau pia kuwa, show hiyo haiwezi kuwa kamilifu
bila kuwepo burudani kali kutoka kwa wasanii wa nyumbani wakiwemo Diamond, AY
na Mwana FA (The Gladiators), Ommy Dimpoz, Chege na Temba, Richie Mavoko,
Vanessa na Gosby, Young Killer ba wengine kibao.
0 comments: