Home
» Enterteinment
» Dayna akizungumzia sakata la beat ya wimbo wake kutumiwa na Diamond kwenye Number 1 (Audio)
Dayna akizungumzia sakata la beat ya wimbo wake kutumiwa na Diamond kwenye Number 1 (Audio)
Apparently wimbo mpya wa Diamond, Number 1 ambao video yake
ilifanyika nchini Afrika Kusini na kuzinduliwa wiki iliyopita, umetumia beat ya
wimbo wa Dayna Nyange uliokuwa umerekodiwa tayari na alipanga amshirikishe
Diamond.
Dayna aliyewahi kuhit na wimbo Nivute Kwako, ameiambia Bongo5
kuwa wimbo huo aliurekodi muda mrefu na alikuwa akimsubiri tu Diamond aingize
sehemu yake lakini mara nyingi haikuwa rahisi kutokana na ubusy wake na tayari
alikuwa amemsikiizisha demo yake.
“Tulisikiliza ule wimbo kwenye gari yake, akasikiliza kama mara
tatu hivi akaniambia ‘kazi ni nzuri tunaweza tukafanya kitu,” anasema Dayna.
“Ni track ambayo nilikuwa naitegemea na nilikuwa
naiamini,”aliongeza.”Ukimuangalia Diamond ni mtu ambaye mimi simfikii kisanaa,
ni mtu ambaye tayari kafika mbali, kwahiyo nilijua hata nikikaa naye kwenye ile
kazi, ni kazi ambayo na mimi ingeweza kunisogeza sehemu fulani.”
Anasema baada ya kumsikilizisha wimbo huo, wakapanga Diamond
akafanya kipande chake lakini ratiba zao zilikuwa zinapishana. Dayna anasema
baada ya muda kupita alikuja kupigiwa simu na mtu aliyedai ameusikia wimbo wa
Diamond uliotumia beat yake lakini hakuamini.
“Kwa mazingira yale tuliyokuwa tumeanza na ile kazi mwanzoni
mpaka kusikia eti nakuja kuambiwa hivyo mimi nilikataa sana.”
Baada ya kushindwa kuamini, mtu huyo alimtumia wimbo huo wa
Diamond kipindi ambacho ulikuwa haujatoka na kuamini kweli beat yake imetumika.
Dayna anasema anakumbuka Diamond hajawahi kwenda kwenye studio ya Sheddy
Clever, producer wa wimbo huo kitendo ambacho anasema kimetokea baada ya kuwa
ameusikia wimbo wa Dayna na kuupenda na hivyo kumfuata producer huyo na
kumshawishi beat aitumie yeye.
“Kwenda kwake kwa Sheddy, alikwenda kitofauti kwamba kwa lengo
la kunizunguka mimi na kwenda kuitumia ile beat,” anasema Dayna.
“Baada
ya kupata uhakika wa hicho kitu kiasi fulani kwanza kilinivunja moyo na
kilinivunja nguvu ya kufanya kitu chochote,” anaelezea Dayna kuhusiana na jinsi
alivyojisikia baada ya kuujua ukweli na hata hivyo anasema hakuweza kumpigia
simu Diamond
Kwasababu kwa upande wangu mimi, nilijiuliza maswali kama
nikimpigia simu Diamond namuuliza, ‘Diamond kwanini umetumia beat yangu’ wakati
najua kweli ametumia beat yangu?” anahoji msanii huyo.
“Kwahiyo mimi sikuweza kumpigia simu tena Diamond na Sheddy kwasababu
nilishawahi kumpigia simu akaniambia kwamba hakijafanyika kitu, kwahiyo nikajua
kabisa hawa walishakaa, wakakubaliana ndo wakaamua kulifanya.
Diamond ni mtu ambaye nilikuwa namheshimu sana na nilikuwa
namkubali sana kutoka moyoni mwangu japo kila mtu na mapungufu yake na
nilimuamini sana kiasi kwamba hiki kitu alichonifanyia yaani kimenivunja moyo
kweli, kimeniuza kweli.”
Amesema kwa sasa kuna ushauri aliopewa kuufanya ili kupata
suluhisho la hicho kilichotokea na atatoa taarifa baadaye.
Wakati huo juhudi za kumpata producer wa wimbo huo, Sheddy
Clever ili azungumzie upande wake zimegonga mwamba kwakuwa hapokei simu zetu na
Diamond yupo nchini Kenya kikazi.