CCM yajipanga kulirejesha jimbo la Iringa Mjini
Chama Cha Mapinduzi Iringa kimeanza mikakati ya kurejesha Jimbo
la Iringa Mjini linaloshikiliwa na Mchungaji Peter Msigwa kupitia
Chadema kwa kutoa mafunzo maalumu kwa wanachama wake.
Mkakati huo umezinduliwa juzi jimboni humo kwa
chama hicho kutoa mafunzo ya siku mbili kwa mabalozi wa nyumba kumi
kuhusu msingi wa chama na mbinu za kulinda uhai wa chama.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo, Salum Madenge
alielezea kushangazwa na ushindi walioupata Chadema kwenye uchaguzi Mkuu
wa 2010 wakati walipata kiti kimoja cha udiwani kutoka katika kata 17
za jimbo hilo.
Madenge alisema umefika wakati sasa kwa mabalozi
kutambua kuwa chama kinaanzia kwao na kwamba wao ni watu muhimu katika
kulinda uhai wa chama, huku akisisitiza kuwa wakitimiza wajibu wao jimbo
hilo litarudi mikononi mwa CCM katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza na wajumbe hao, Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa (Nec) anayewakilisha Wilaya ya Iringa, Mahamoud Madenge
alisema wanachama wa (CCM) Jimbo la Iringa Mjini walifanya kosa kwa
kuacha kuchagua chama chao na kupigia kura upinzani