Serikali yatangaza nafasi za kazi 1,134.
Serikali
kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
inawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza nafasi wazi za kazi
kama zilivyo katika Tangazo la Lugha ya Kiingereza na Kiswahili.
Kwa
mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.
Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya
Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya Waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.
Daudi alifafanua kuwa Waajiri hao ni pamoja na
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu
Mkuu wizaraya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Afisa
Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, Katibu Mkuu
Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda
na Biashara. Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Katibu Mkuu Wizara
ya Maji, Katibu Ofisi ya Rais Maadili,
Wengine ni Katibu Tawala
wa Mkoa Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Manyara, Dar
es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani, Mara, Kilimanjaro, Lindi, Singida,
Tabora, Tanga, Katavi na Arusha, Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la
Mwanza, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Iringa, Songea, Shinyanga,
Morogoro, Singida, Kigoma/Ujiji na Temeke.
Nafasi
nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mufindi,
Kyela, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba, Namtumbo,
Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe, Sengerema,
Ilemela, Busega, Maswa, Meatu, Shinyanga, Kishapu, Kilosa, Msalala,
Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli,
Ngorongoro,Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora,
Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto, Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino,
Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa naTandahimba. Mkurugenzi Halmashauri
ya Mji Njombe, Kibaha, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na TEMESA.
Katibu
huyo amesema kuwa nafasi hizo zilizotangazwa zimegawanyika katika kada
zifuatazo; Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta daraja la II – (Nafasi 10),
Afisa Vipimo II – Nafasi 6, Mpima Ardhi daraja la II (Nafasi 26),
Mhandisi daraja la II – Ufundi Umeme – Nafasi 9, Afisa Mipango Miji
daraja la II– Nafasi 13, Mhandisi daraja la II - Ujenzi (Nafasi 16),
Mhandisi daraja la II - Maji (Nafasi 13), Afisa Misitu daraja la II
(Nafasi 7), Afisa wa Sheria daraja la II – nafasi 3, Mtakwimu Daraja la
II – nafasi 8, Mthamini daraja la II – Nafasi 7, Mkadiriaji Ujenzi
daraja la II – nafasi 4, Afisa Ufugaji Nyuki Daraja la II – nafasi 1,
Mhandisi Daraja la II – Nishati (Nafasi 3), Msanifu Majengo Daraja la
II– (nafasi 3) na Mjiolojia Daraja la II – Nafasi 7, Fundi Sanifu daraja
la II (Ujenzi) -Nafasi
26, Mvuvi Msaidizi Daraja la II – nafasi 8 na Fundi Sanifu Msaidizi (Maji) -nafasi 19.
Nafasi
nyingine zilitotangazwa na Serikali ni Nahodha Daraja la II – Nafasi 6,
Fundi Sanifu daraja la II - Haidrolojia -Nafasi 6 ,Fundi Sanifu Daraja
la II -Nafasi 6, Msaidizi Misitu Daraja la II – nafasi 7, Fundi Sanifu
Daraja II – Ramani – Nafasi 6, Fundi Sanifu Daraja la II –Maendeleo ya
Jamii– Nafasi 3, Dereva Mitambo Daraja la II– nafasi 1, Mpiga chapa
msaidizi- Nafasi 5, Operata wa kompyuta msaidizi - nafasi 3, Fundi
Sanifu Daraja la II - Migodi – nafasi 9, Polisi Msaidizi– Nafasi 5,
Mpokezi–Nafasi 1, Katibu Mahsusi daraja la III-nafasi 10, Mlinzi –Nafasi
100, Dereva Daraja la II – nafasi 178, Msaidizi wa Ofisi– Nafasi 30,
Afisa Kumbukumbu daraja la II– nafasi 1, Mwenyekiti wa Mabaraza ya
Ardhi na Nyumba ya Wilaya – nafasi 5, Afisa Mtendaji wa Kata Daraja la
III– nafasi 10, Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la II– nafasi 6.
Aidha,
kada nyingine ni Afisa Mtendaji wa Kijiji daraja la III) – nafasi 232,
Afisa Mtendaji Mtaa daraja la III– nafasi 3, Afisa Lishe daraja la II–
nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II - Ufundi na Umeme, Afisa Biashara
msaidizi– Nafasi 1, Mchapa Hati daraja la II – Nafasi 1, Mhandisi
Daraja la II –Baharini-(nafasi 1), Dereva Mitambo Daraja la II – (nafasi
1), Dereva wa Vivuko daraja la II – Nafasi 3, Mkufunzi Mwandamizi
Daraja II - Nafasi 1, Mkufunzi Daraja ii - Nafasi 2, Fundi Sanifu
Msaidizi (bomba)–nafasi 3, Fundi Sanifu Msaidizi (Umeme) –Nafasi 4,
Mkufunzi Daraja II– nafasi 3, Mkufunzi daraja la II -Jiolojia – nafasi
1, Mkufunzi Msaidizi– Jiolojia – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja II
-Ubunifu Mipango Miji – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja II- Urasimu Ramani
– Nafasi 5, Fundi Sanifu daraja II- Uchapaji Ramani –Nafasi 4, Fundi
Sanifu Daraja la II -Maabara– nafasi 13, Fundi Sanifu Msaidizi (Ujenzi–
nafasi 1), Fundi Sanifu daraja la II -Nafasi 4, Wakufunzi wasaidizi –
nafasi 54 na Mhasibu Mkuu daraja II.
Katibu alifafanua kuwa
nafasi 949 zilizoko katika tangazo la Kiswahili ni kwa ajili ya Waajiri
walioainishwa hapo juu na kwa Tangazo la nafasi wazi 185 zilizoko katika
tangazo la lugha ya Kiingereza ni kwa ajili ya Taasisi na Wakala
mbalimbali za Serikali.
Daudi amesema mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 9 Aprili, 2013.
Aidha,
amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kufungua matangazo yote
mawili ya kazi na kuzingatia masharti ya Matangazo yote kama yalivyo
katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili kabla ya kutuma maombi yao.