Msemaji kampuni ya Weusi, Nick wa Pili amesema kuwa rapper
Lord Eyez amesimamishwa na kampuni hiyo kutokana na kuvunja maadili.
Nick wa Pili amesema baada ya kupokea taarifa za Lord Eyez
kushikiliwa na polisi huko Arusha kwa wizi wa Laptop walikaa kikao na kuamua
kumsimamisha.
“Kitu ambacho naweza kusema kutoka Weusi ni kwamba Lord Eyez
tumemsimamisha kazi kikampuni,” Nick ameiambia Bongo5. “Uamuzi wa kumsimamisha
tumeufikia jana na leo ndio tumeamua kutangaza rasmi kwamba Lord Eyez
tumemsimamisha kazi na amesimamishwa kutokana na misingi na makubaliano ya
kampuni,kulingana na maadili ya kampuni yetu na mawazo yetu kwa pamoja ndio
yamefanya tukamsimamisha. Kwahiyo ni kwamba tumemsimamisha kutokana na
makubaliano ambayo yalifikiwa ndani ya kampuni ambayo mengine yatabakia ndani
ya kampuni.”
Uamuzi huo wa Weusi umekuja kufuatia taarifa kuwa Lord Eyez
alikamatwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa laptop Jumamosi, huko Arusha na
baadhi ya picha za tukio hilo kuonekana. Taarifa hizo zimedai kuwa anatuhumiwa
kwa wizi wa laptop aina ya ‘Dell’.
Mwaka juzi, Lord Eyez alikamatwa na kufikishwa mahakamani
kwa tuhuma za wizi wa Power Window za gari la Ommy Dimpoz, lakini Ommy
alitangaza kumsamehe msanii huyo.
0 comments: