MASTAA NA WADAU WA SANAA WAPINGA UDHALILISHWAJI ALIOFANYIWA PNC, YEYE ASEMA ‘POTELEA MBALI’

Kitendo cha udhalilishwaji alichofanyiwa msanii Pancras Ndaki Charles aka PNC na meneja wake Ostaz Juma wa Mtanashati Entertainment, cha kumrekodi msanii huyo akiwa amempigia magoti akimuomba msamaha kisha kusambaza picha na clip ya video mtandaoni kimewasikitisha wengi.
Kitendo hicho kimewakera wadau wengi wa sanaa ambao wamedai kuwa alichokifanya Ostaz sio sahihi na ni ishara ya unyanyasaji.

Kupitia ukurasa wake wa facebook jana (Feb 26) Ostaz aliweka picha na video inayomuonesha PNC aliyekuwa akimsimamia na kuandika:


“hahaha jamani mziki ni kazi…pnc arudi kuomba msamaha ili aendelee kufanya kazi mtanashati.”

Haya ni baadhi ya maoni ya mastaa na wadau wengine wa sanaa wanaopinga kitendo hicho:

Adam Juma wa Visual lab/Next Level:
 Sanaa ina thamani gani katika jamii? Wengi wanaichukulia sanaa kama upotezaji muda tu, wengi hawaithamini sanaa kabisa. Na sizungumziii sanaa ya kuimba tu bali sanaa zote, hata kupiga filamu, kutaarisha mziki au uchoraji ni moja ya sanaa na inahitaji umahiri. Jamii yetu kwa ujumla haitupi sifa wanasanaa tunazostahili, sipendi mtu akinichukulia mimi kama “ MPIGA VIDEOOO” huku akiongea na mimi kwa fedheha kisa anauwezo wakulipa, kamwe huwezi kumlipa msanii naomba litambulike hilo. Pia litambulike kuna watu wameeacha kazi zao ambazo walipata mpaka madegree wakaamua kufanya sanaa, kwahiyo sio kila anayefanya sanaa ana njaa au anafanya kwa shinda. Mimi binafsi maisha yangu na yafamilia yangu yaendeshwa kwa kutumia sanaa. Mtu akinidharau kamwe sifanyi nae kazi hata kama anamipesa Hivi leo polisi akitukanwe hadharani kutakua na usalama, polisi wengine hawatakubali? Hivi mtu amdhalilishe dereva wa boda boda unafikiri ni sawa? Kwanini mtu amdhalilishe msanii alafu wana sanaa wote mnakaa kimya kama hayawahusu vile. Mimi PNC sio msanii wangu, lakini naheshimu kazi zake na jitihada zake kama msanii, mimi kama msanii naamini yeye kama msanii amepitia changamoto mpaka amefikia hapo alipo. Naamini huyu msanii ana wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wanamtazama, hivi wanamchukuliaje huyu msanii kwa kudhalilishwa mbele ya umma. Baada ya kupata taswira hiyo vuta picha nyingine wanaichukuliaje sanaa kwa ujumla kama mtu anaweza akamfanya msanii hiyvo na asifanywe lolote, maana yake ni sanaa haina thamani. OSTADHI JUMA umeikosea sanaa, umewakosea wanasanaa wote na kama wewe ni msanii basi hustahili sifa hiyo ya usanii. Muombe radhi huyo kijana na jamii nzima ili ulinde heshima yako iliyobaki na heshima ya sanaa kwa ujumla.

Said Fella:
 Sijaielewa hii picha wadau hivi nikweli tz au nje ya nchi shino na meneja wake wa mziki huu wa bongo frevar jamani mnao hitaji kujifunza umeneja naomba mnitafute niwafundishe busara kuusu mziki kweli vijana wetu (wasanii)kuna mda wanazingua lakini tusitumie nguvu ya mifuko yetu kudhalilisha wenzetu milango nimeiacha wazi mje mjifunze

Baada ya watu kuchangia katika alichokiandika Fella Instagram, Ostaz Juma ali-comment kwa kuandika, “hahahaha nampenda sana,juma nature mkubwa tufanye mpango wa kumumeneji juma nature”.

Suma Mnazaleti:
 Cjapendezwa ata kidogo Na kitendo alichofanyiwa msanii uyu PNC Na Ostadh Juma Na musoma baada ya kwenda kumuomba samahan! Ichi ndicho alichofanyiwa kupigishwa magoti Na kupigwa Picha Na kurecodiwa clip ya video. Tazama Picha hii we kama shabiki Wa bongo fleva huu c udharirishaji? Huu c utumwa kabisa? Mziki ulikuwa ni sehem ya vijana wenye vipaj kujipatia ajira nw unaelekea kuwa sehem ya wapenda CFA wachache wenye visent vya magumash kuwanyanyasia vijana wadogo waliotoka kwnye familia za kimaskini Na Vipaj vyao! Je we kama shabiki Wa msanii uyu maarufu kwa hali hii unayoiona hapo utamueshm kweli Na kumpa thaman kama zaman? Au we kama Ndo ungekuwa msanii uyo baada ya kufanywa hvyo, uyo jamaa anaweza kuwa boss wako kweli? Cwez kumlaumu PNC kwa sbb ana kitu Ndo maana alikubali kufanywa hvyo! Ila we ungependa kuona mziki Wa bongo fleva Na wasanii wanaojipatia majina makubwa nchini mwishon wakiishia kufanywa HV Na wapenda CFA?

Mike Tee:
 Msanii mwenzangu PNC kadhalilishwa sana na OSTADH JUMA kwenye MEDIA zote, me toka jana natafakari sana kwa mtu mzima kufanya kitendo kama kile, upande wangu nimeumia na nimeona kama mimi nimefanyiwa kitendo kile.
 Sasa basi wasanii wenzangu, washabiki wetu , viongozi wa ngazi mbalimbali tunajua mambo haya yapo lakini yana kipimo, tukikaa kimya wako watakaotuvua nguo hadharani kisa sisi wasanii ambao tunadharaurika hatuna elimu hatuna kipato ila tunatumika na wachache kupata wanachotaka,
 Je tufanye nini me nimeshindwa cha kufanya we need your support wenye uchungu wa muziki wetu na wasanii wa TANZANIA kwa ujumla.

Kitale:
 Pole PNC hayo Ndio maisha kama mama yako au baba yako alishawaigi kukuambia au mtu yyte aliwahai kukuambia basi Ndio hayo maisha yenyewe ni njia moja wapo ya mafanikio.

Alawi Junior:
 UKIHISI UMEMKOSEA BABA AU MAMA OR FAMILY KIUJUMLA SIO DHAMBI KUPIGA GOTI KUOMBA SAMAHANI LAKINI UNAMPIGIA GOTI MTU AMBAYE ANATAKA UMUIMBE AKULIPIE VIDEO MIL 2 APATE UJIKO NI UJINGA HUO.. ARTIST WA UKWELI HAWEZI KUFANYA HVYO ULIVYOFANYA UMECHEMKA MDOGO WANGU JIVUNIE KIPAJI CHAKO..AM DONE

Mkwaby Hassani:
 Kakosea sana na sio vizur kupata kwake yey co iwe fimbo kwa wanyonge kama iv kamdharirisha sana ubnadam hana uyu jamaa co kumpga pcha mtu iv inamaana yey ajawai kosea? Au atokuja kosea kamwe afikilie mara 2 maisha mafup sana akumbuke islaer anamdai xo asirizke ivyo CHEFUA SANA WATU araf yy anaona SIIIFA KUBAF

Hellen kazimoto:
 Daaah is not fear at all. Meneja haezi mzalilisha msanii wake this much. Kulikua hakuna haja ya kumpga pcha akiomba samahani otherwise huyu anaejiita meneja anatafuta umaarufu mavi. …so stupid sio fear mkubwa wafundishe kazi wasikurupuke.

Hata hivyo akiongea na tovuti ya Times FM, PNC amesema haoni kama ni tatizo kwake kufanya hivyo.

 Mimi naweza nikasema ni kawaida tu, kwa sababu kuomba msamaha pia ni kitu cha kawaida sio tatizo. Mimi nimefanya hivyo kwa maana yangu tu najua mwenyewe nimefanya hivyo kwa sababu bado nahitaji kufanya kazi zangu ziende. Kwa hiyo sasa nikisema niwe kiburi nini…japokuwa sijakosa mimi ila mkubwa anapoona kuna makosa akawajumlisha wote inabidi mjishushe saa nyingine, ujichukulie kama mdogo sio na wewe unaanza kuwa una viburi na jeuri. Nimeshakaa kwenye game…muziki nimeuanza muda najua madhara yake ni yapi. Kwa hiyo nimefanya tu kawaida kumwambia bwana mambo haya yaishe na nini tufanye mambo yetu.

Kwa sababu yeye mwenyewe kitu kilichokuwa kinaongeleka kwake ni lawama zake kwamba mimi nilimletea watu, mwisho wa siku wamekuja kuharibu mambo yake mpaka wanafikia hatua ya kufanya mambo mengine wanamkana na nini. Sasa mimi ukiangalia ukweli mimi ndiye niliyewakaribisha wasanii wote waliokuwa Mtanashati. Lakini sio kwamba mimi ndio niliyekosea kwamba nilikosea…mimi sikugombana na Ostaz ila niliona kimya nikaanza kuona hapa kazi hazieleweki nikaamua kusema kama vipi siko Mtanashati. Ila mwisho wa siku nikaa kuongea nae nikajua tatizo liko wapi. Kwa hiyo ikabidi nimweleze bana kama vipi basi tusameheane mambo hayo yaishe tufanye kazi.

Ukiangalia kwenye hizi picha, nimeziona hizi picha na kuna watu wanaandika mambo yao ya ajabu ajabu wanadiss, lakini mimi naona sawa tu kwa sababu kupiga goti na kumuomba mtu msamaha sio kwamba umemsujudia yeye ndio Mungu hakuna. Ni kama umeonesha heshima tu kwamba wewe ni brother. Ukiangalia mimi silingani nae umri hata kidogo na huyo mtu ndio mtu ambaye hata kwa ndugu zangu anaongea nao. Kwa hiyo fresh tu nimeomba samahani kama brother angu. Potelea mbali maneno yataongeleka yataenda yatapita, mimi kazi zangu ntaendelea kufanya.

0 comments:

Post a Comment

Recent Posts