Home
» Habari za Kitaifa
» MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI IDODI AMELAZWA BAADA YA KUTANDIKWA VIBOKO 100 NA MWALIMU
MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI IDODI AMELAZWA BAADA YA KUTANDIKWA VIBOKO 100 NA MWALIMU
Mwanafunzi
wa shule ya sekondari Idodi wilayani Iringa amelazwa katika Hospitali
ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa madai ya kupigwa viboko zaidi ya 100 na
mtu anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule hiyo na kufungiwa katika bweni
kwa siku 3 ili kuificha siri hiyo.
Tukio hilo linakuja wakati harakati mbalimbali za kijamii na asasi za kiraia zikipiga kelele kupinga vitendo vya ukatili wakati jeshi la Polisi likianzisha dawati la jinsia kwa ajili ya kutokomeza masuala hayo.
Ni mwanafunzi Lusinde Nyaulingo, wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Idodi, ambaye anaugulia maumivu makali katika Hospitali hii ya rufaa ya mkoa wa Iringa, word namba tano ya majeruhi, kutokana na ukatili uliosababisha majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake, hasa maeneo ya mapaja, makalio na mgongo, baada ya kupigwa kwa tuhuma za kuchukua simu ya mwanafunzo mwenzie, jambo linalomfanya mwanafunzi huyu apoteze muda mwingi wa masomo wakati akipatiwa matibabu ili kurudisha afya yake.
Lusinde anasema baada ya kuangushiwa kipigo hicho kikali, kilichodumu kwa zaidi ya masaa tatatu, alipoteza fahamu na kisha kufungiwa katika bweni kwa siku tatu, huku wanafunzi wenzie wakipigwa marufuku kufikisha taarifa ya ugonjwa kwa wazazi wa Lusinde.
Hata hivyo jeshi la polisi kupitia kamanda wake mkoa wa Iringa ACP Athmani Mungi limesema kuwa wanafuatilia tukio hilo ili kuhakikisha haki inatendeka, kwa kumchukulia hatua za kisheria mtuhumiwa ikiwa ni pamoja na kumfikisha Mahakamani.
-Star tv

You may also Like

NAIBU WAZIRI WA AFYA WA ZAMANI LUCY NKYA ADAIWA KURUSHIANA R...

Chidi Benz akamatwa na dawa za kulevya airport...

Hii ndio historia ya mziki ya mareheme YP kutoka TMK Wanaume...

IPHONE 6 NA 6 PLUS MILIONI 10 ZIMESHANUNULIWA HADI SASA!...

Maharusi waoana ndani ya bwawa la maji...

Rapper Navio ambaye yupo Bongo asema anatamani kufanya colla...
Followers
Tags 2
Popular Posts
-
Vijana wa Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova kwa kushirikiana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) wamefani...
0 comments: