Muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba Tanzani kurudishwa bungeni.

 Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania  na viongozi wa vyama vya siasa vya CCM, Chadema, CUF, NCCR- Mageuzi, TLP na UDP wamekubaliana kuwa kuna upungufu katika sharia ya mabadiliko ya katiba walipokutana Jumanne katika  Ikulu ya Dar es Salaam.
Mkutano huo ambao uliitishwa na Rais Kikwete ulitokana na wabunge wa vyama upinzani kutoa kauli ya kutaka  kuandamana baada ya bunge kupitisha mswaada wa sheria ya mabadiliko ya katiba bunge lilipokutana Dodoma mwezi Septemba.
Rais Kikwete alikubali kwamba lazima wakae wazungumze akitolea mfano wa siku za nyuma.
mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Chadema Freeman Mbowe amesema Rais Kikwete ametoa mwito wa kutafuta ufumbuzi wa pamoja na ndicho walichofanya huko Ikulu.
Mambo ya msingi waliyokubaliana ni kwamba sheria ina mapungufu na itabidi wairudishe bungeni ifanyiwe mabadiliko.
Wamekubaliana pia wasikilize maoni ya wadau wa Zanzibar. Kuhusu hoja ya mchakato wa katiba uwe shirikishi na   usihodhiwe na chama chochote cha siasa, sababu tabia ya wabunge wa CCM kujiona wana haki ya ziada kuliko raia wengine kuhodhi mchakato wa katiba haukubaliki kwani inaweza kupelekea taifa kwenye machafuko.
Wabunge wa vyama vya Chadema ,CUF na NCCR Mageuzi walisusia mjadala wa mswaada huo wakipinga kuwa utaratibu uliotumika haukushirikisha  upande wa Zanzibar na pia walikuwa hawakubaliani na baadhi ya vipengele vya mswaada huo.

0 comments:

Post a Comment

Recent Posts