JACKSON KISWAGA AWALIPIA WAKAZI 30 KATIKA MFUKO WA AFYA VIJIJINI CHF

Mkazi wa kijiji cha Nyamihuu, kata ya Nzihi tarafa ya Kalenga mkoa wa Iringa Bw. Jackson Kiswaga ametoa msaada wa kulipia kaya 30 katika mfuko wa afya vijijini (CHF) alioanzishwa na serikali. Amesema amelazimika kutoa msaada huo baada ya kuombwa na serikali ya kijiji cha Nyamihuu kusaidia familia zinazoishi katika mazingira magumu. Wakati wa kukabidhi msaada kwenye kamati ya kijiji inayoshughulikia masuala ya afya amesema ‘’afya na mali na utajiri’’ kwa ameipongeza serikali kwa juhudi za makusudi za kuwapunguzia wananchi mzigi kwa kuanzisha huduma hii ya afya ambapo kaya moja huchangia asilia 50% na serikali nayo hutoa 50% na kuiwezesha familia husika kutibiwa kwa mwaka mmoja bure katika zahanati za serikali.
Mzee Lasiang’ombe Mbembe mwenyekiti wa CCM kijiji cha Nyamihuu amempongeza sana Bw. Kiswaga na kumwelezea kuwa na kijana wa kipekee sana. Amesema kwa miaka kadhaa sasa amekuwa msaaada na mshauri mkubwa kijijini hapo. Ukiacha msaada baiskeri aliotoa mwaka juzi kwenye serikali ya kijiji, kuchangia ujenzi wa nyumba ya waalimu, madawati na kusomesha watoto watatu katika shule ya kata Kidamili, pia amekuwa akifanya mpango wa upatikanaji wa maji. Mzee Mbembe amesema ikiwa kijiji kitapata vijana kumi kama Jackson Kiswaga basi Nyamihuu watakuwa peponi. Yeye mwenyewe Kiswaga amesema nia yake ni kusaidia familia zote zitakazothibitishwa na uongozi wa kijiji kuwa hazina uwezo na mpango wake mpana na kusaidia familia kama 1000 mkoa wote wa Iringa.
 
Taarifa na Godwin Francis.

0 comments:

Post a Comment

Recent Posts