Home » Unlabelled » IRINGA: POLISI WAFANIKIWA KURUDISHA ASILIMIA KUBWA YA FEDHA ZILIZOKUWA ZIMEPOLWA NA MAJAMBAZI.
IRINGA: POLISI WAFANIKIWA KURUDISHA ASILIMIA KUBWA YA FEDHA ZILIZOKUWA ZIMEPOLWA NA MAJAMBAZI.
hilingi Milioni 80 ambazo zimerejeshwa na jeshi la polisi kutoka mikononi wa majambazi wa tukio la utekaji wa raia wa Kichina, waliovamiwa katika mlima wa Nyang'olo mkoani Iringa. |
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Iringa ACP Athmani Mungi amesema raia hao wa china wa kampuni ya SIETCO, inayojenga barabara ya Iringa- Dodoma, walikutwa na mkasa huo wakati wakirejea kutoka Iringa mjini, ambapo msako mkali wa jeshi hilo umefanikisha kupatikana kwa shilingi Milioni 80.
ACP Mungi amesema wachina hao walitekwa na kuporwa kiasi hicho cha fedha na vitu mbalimbali, mara baada ya kuchukua fedha hizo katika benki ya CRDB tawi la Iringa, na wakiwa katika gari lao aina ya Toyota yenye namba za usajili T. 335 CMX lilizuiliwa na gari kubwa aina ya Lori katika mlima wa Nyang'olo huku watu watano wenye siraha wakapora mfuko uliokuwa na fedha hizo.
Amesema majambazi hao walichukua pia simu za mkononi tano na funguo za gari la wachina na kutokomea nalo pamoja na kiasi hicho cha fedha cha shilingi Milioni 135, ambazo walikuwa wanarudi
nazo katika kambi yao ya Mtera.
"Wachina hao walikuwa wametoka kuchukua fedha hizo katika benki ya CRDB tawi la Iringa mjini bila kuwa na ulinzi wowote wa askari Polisi, na walikuwa wanazipeleka katika kambi yao iliyopo
Mtera," Alisema Mungi.
Amesema jeshi la polisi baada ya kupata taarifa hiyo walifanya oparesheni la kuwasaka majambazi hao mchana na usiku, kwa kushirikiana na wananchi wa vijiji vya tarafa ya Isimani, ambapo zoezi hilo liliendelea mpaka siku ya tarehe 23 alfajiri walipowaona majambazi hao.
Mtera," Alisema Mungi.
Amesema jeshi la polisi baada ya kupata taarifa hiyo walifanya oparesheni la kuwasaka majambazi hao mchana na usiku, kwa kushirikiana na wananchi wa vijiji vya tarafa ya Isimani, ambapo zoezi hilo liliendelea mpaka siku ya tarehe 23 alfajiri walipowaona majambazi hao.
You may also Like
Followers
Tags 2
Popular Posts
-
New AUDIO | Geez Mabovu - Story | Download Sikiliza & Download Nyimbo ya Marehemu GEEZ MABOVU akiwa amemshirikisha GALATONE
0 comments: