Diamond atangaza ndoa
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platinumz ametangaza ndoa na
mchumba wake wa muda mrefu Wema Sepetu anayosema itafungwa hivi
karibuni.
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza
na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano.
Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo
maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.
“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo
mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo
hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.
Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi
nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi,
tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka
tuje kuwa mfano wa kuigwa.”
Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi
karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima
uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri,
lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa.
Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.”
Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba
wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali huyo wa wimbo ‘Mdogo
Mdogo’
“Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo,
nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu
nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa
haonekani lakini anayemaliza.
Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema.
Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.
“Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi yanavyoandika, wakati
mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha baraza,” aliongeza.
Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake huyo, alisema:
“Hatuna tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini hatujaachana na
hatuwezi kujibishana.
“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu”
Na Mwanaspoti.
0 comments: