Home
» Video
» Video: Diamond aelezea walichozungumza na meneja wa Trey Songz, Kevin Liles alipokutanishwa naye na Rais Kikwete Marekani
Video: Diamond aelezea walichozungumza na meneja wa Trey Songz, Kevin Liles alipokutanishwa naye na Rais Kikwete Marekani
Hivi karibuni Diamond Platnumz alipata nafasi ya kukutana na
mtu mkubwa katika industry ya muziki wa Marekani Kevin Liles, ambaye ni rais wa
zamani wa Def Jam na kwasasa ni meneja wa muimbaji wa R&B Trey Songz na Big
Sean.
Bongo5 ilitua Durban kwaajili ya Tuzo za MTV MAMA
zilizofanyika Jumamosi iliyopita, ilipata nafasi ya kufanya Exclusive Interview
na Diamond kabla ya tuzo hizo, pamoja na mengine Platnumz ameelezea
walichozungumza alipokutanishwa na Liles na Rais Kikwete nchini Marekani.
“Ilikuwa ni namna ya kuangalia nafanya vipi katika soko la
Amerika na dunia nzima” Alisema Diamond. “So nilipokutana na Mheshimiwa Rais
akaniambia kitu gani unahitaji nikusaidie, nikamwambia connection, kila kitu ni
connection njia ya kuweza kuingia katika soko la Amerika na dunia nzima, so
akasema basi nitakukutanisha na mtu fulani ambaye naamini anaweza akakusaidia,
so akamtafuta akampigia simu nikaonana naye(Kevin Liles)”.
Akizungumzia jinsi
alivyo busy sasa hasa katika kujitangaza kimataifa:
“Nimekuwa nikienda speed sana kiukweli nimekuwa nikizunguka
usiku na mchana kutafuta connection…wanasema wakati unapopatikana utumie vizuri
hapo hapo unapopata sehemu hata kama kuna magoli mia piga hapo hapo mapumziko
utapumzika baadae.”
Kuhusu collabo aliyoifanya na Mafikizolo:
“Nadhani kila mtu atakuwa na rights kwa upande lets say East
Afrika nitakuwa na haki nayo mimi South Afrika wao, ikienda West ttakuwa
tunagawana labda”.
Kuhusu wimbo mpya aliomshirikisha Iyanya na video yake
kufanyika na director Mnigeria Mr Moe Musa, Diamond amesema video bado
haijatoka japo imeanza kuchezwa Channel O.
“Video kiukweli kutoka bado tho nimeambiwa kuna Channel
imeanza kupigwa (Channel O) sio mbaya lakini bado haijakuwa official released
nitawaambia”. alisema Platnumz aka Chibu!
Leo Alhamisi (June 12) Diamond atatambulisha rasmi single
yake mpya ‘Mdogo mdogo, ambayo hapo awali ilivuja kwa jina la ‘Kitorondo’.
0 comments: