Home
» Local News
» Mume wa Florah Mbasha anena kuhusu tuhuma za kumbaka shemeji yake
Mume wa Florah Mbasha anena kuhusu tuhuma za kumbaka shemeji yake
Stori: Sifael Paul na MAKONGORO OGING’
Upande wa pili wa shilingi! Kwa mara ya kwanza tangu ahusishwe na skendo
ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17, mume wa mwimbaji wa
Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha ameibuka na kuzungumza na
Uwazi katika mahojiano maalum dhidi ya kashfa yake hiyo huku akitishia
kujiua.
Akizungumza kwa njia ya simu kwa zaidi ya saa moja mwishoni mwa wiki
iliyopita huku akikanusha kukimbilia mafichoni baada ya kuondoka
nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar hivi karibuni, Mbasha ambaye pia ni
mwimba Injili kama mkewe, alianika kila kitu akidai cha siri kwamba
anajua anachezewa mchezo mchafu baada kuwepo kwa gogoro zito kati yake
na mkewe hadi kutishia uhai wa ndoa yao.
ASIMULIA TUHUMA
“Tuhuma zilizoripotiwa na binti aitwaye... (anamtaja jina) ambaye kweli
ni ndugu wa mke wangu (Flora) kwenye Kituo cha Polisi Tabata-Shule (Dar)
si za kweli.
“Anayefanya mambo hayo yote ni mke wangu, anataka nipotee ili awe huru. Mimi najua hilo.”
KASHFA YA KUTENGENEZA
“Hii kashfa ni ya kutengeneza ili nipotee lakini sipo tayari kupata aibu, bora nijiue.
“Mke wangu amekuwa tatizo kwenye ndoa yetu.
“Kweli ndoa yangu na Flora ina matatizo lakini matatizo yetu ya ndani
sana hakuwa na sababu ya ‘kuinjinia’ mpango mchafu wa kunimalizia
gerezani mimi ili yeye aponde raha.
“Nyuma ya haya mambo kuna vitu mtu ukivisema ni aibu sana kwa upande wa pili. Lakini navijua.”
MKE ALIONDOKA NYUMBANI
“Mke wangu aliondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini. Hebu fikiria
hapo. Mwanzo alianza kwenda ‘gym’ saa 11:00 alfajiri na kurudi saa 4:00
asubuhi. Pia saa 10:00 jioni aliondoka tenda kwenda gym akawa anarudi
kati ya saa 3:00 hadi 4:00 usiku.
“Nilipomuuliza alinijibu kuwa ni kwa sababu anatembea umbali mrefu. Hebu
ona sababu ilivyo dhaifu jamani! Hata kama ungekuwa wewe mwandishi,
unaonaje?”
“Mimi ni mtu maarufu, ningetaka mwanamke ningepata, iweje nibake?
“Jaribu kufikiria, katika tatizo kubwa kama hili ambalo linaweza
kunifanya nifungwe, nilitarajia mke wangu awe upande wangu, lakini cha
ajabu yeye ndiye amekuwa nyuma ya adui zangu, niamini nini mimi zaidi ya
yeye kuhusika na kuniangamiza?”
“Hausigeli wangu ni mzuri, kwa nini nisimbake yeye?”
AFUATILIA
“Nilipofuatilia niligundua tayari kuna tatizo kwenye ndoa yetu. Mdudu
alikuwa ameingia ndani ya ndoa kwani hadi sasa mke wangu siishi naye.
Anaishi hotelini.
“Anachokifanya mke wangu ni kitu kibaya mno. Alimtengeza yule binti
ambaye nilikuwa namsomesha sekondari pale (anataja shule maarufu Dar),
akampa semina ya kutosha kwamba aseme nimembaka ili nipate misukosuko na
yeye awe huru.
“Kama hiyo haitoshi, akala dili na madaktari, wakafoji majibu ya vipimo
vikionesha kweli yule binti ameingiliwa, sasa sijui kama vipimo
vilioneshaje kama ni mimi.
“Ukweli ni kwamba siwezi kuvumilia kuona napandishiwa kizimbani kwa jambo la kutengenezewa.
“Napiga picha nitakapofikishwa mahakamani jinsi ambavyo vyombo vya
habari vitakavyoandika na picha zangu kwa kesi ya ubakaji ambayo si ya
kweli.
“Dah! Inaniuma sana. Mke wangu nimemfanyia vitu vingi sana. Hakustahili
kunitendea ubaya huu. Alikuwa hafahamiani na mtu yeyote mkubwa. Mimi
ndiye nimempeleka kwa watu wakubwa wakamsaidia sasa amenigeuka, siamini.
Narudia tena, heri kufa kuliko fedheha hii,” alisema Mbasha kwa
uchungu.
HAYUKO MAFICHONI
Kuhusu kuwa mafichoni, Mbasha alisema: “Sipo mafichoni, sijaambiwa na
mtu yeyote nikatoe maelezo polisi. Nipo nimejaa tele, nikiambiwa
nahitajika nitakwenda kutoa maelezo yangu kwani sijawahi kutenda kosa
hilo na Mungu awe shahidi yangu.”
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Dar, Marietha Minangi alithibisha
kuwepo kwa ishu hiyo na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea.
Flora na Mbasha walifunga ndoa Agosti 22, 2002 hivyo mwaka huu
wametimiza miaka 12 wakiwa pamoja ambapo mtoto wao wa kwanza anaitwa
Elizabeth.
0 comments: