Home
» Enterteinment
» Exclusive: Pesa iliyotumika kwenye video mpya ya Diamond na Iyanya London, kolabo na Davido tena?
Exclusive: Pesa iliyotumika kwenye video mpya ya Diamond na Iyanya London, kolabo na Davido tena?
Wiki iliyopita Diamond Platnumz alikua London Uingereza kwa ajili ya
kufanya show lakini pia vilevile kufanya video ya wimbo wake aliofanya
na msanii Iyanya wa Nigeria.
AyoTV na millardayo.com zimepata
Exclusive interview na meneja Babtale ambae anasimamia kazi za Diamond
sasa hivi ambapo amesema kutokana na kupiga hatua kwa Diamond na kuingia
kwenye levo za kimataifa, imebidi waanze kufanya video za kiwango hicho
cha kimataifa lakini haimaanishi kwamba ndio Platnumz hatofanya tena
video Tanzania’
Namkariri Tale akisema ‘video tuliyofanya na Iyanya Uingereza ni kwa
sababu tulikua tunamuhitaji Director MoE Musa ambae anaishi na kufanya
kazi zake Uingereza ndio maana tukasafiri mpaka huko, kuna video ambayo
tutafanya Nigeria tukishatoka Ghana na pia ikitokea kwamba tunatakiwa
kufanya video Tanzania tutafanya hivyo’
Bab Tale: ‘kiukweli tunaumia,
tunaumia kwa sababu kumlipa Moe Musa na kupata kila kitu kama kwenye hii
video ya juzi tumemlipa Moe peke yake dola elfu 25 ambazo zinagonga
mpaka milioni 40 za Kitanzania, bado usisahau tumewatoa kina Iyanya
Nigeria kwa hela yetu kuwaleta London, kuwalipia nauli ya business class
kwenye ndege na hoteli hawawezi kulala hoteli mbaya kama sisi watoto wa
Manzese’
Kwenye sentensi nyingine, Babtale ameithibitishia millardayo.com na AyoTV
kwamba Diamond atasikika tena kwenye kolabo nyingine na Davido
itakayowahusisha pia Tiwa Savage wa Nigeria na Mafikizolo wa South
Africa ikiwa ni kampeni ya kituo kimoja kikubwa cha TV Afrika.
0 comments: