DUDU BAYA AMKATA SIKIO MAMA YAKE MKUBWA AKIDAI NI MCHAWI, ANATAFUTWA NA POLISI


Akizungumza na ‘You Heard’ ya Clouds FM jana mdogo wake wa tumbo moja na Dudu Baya, Mueta amesema juzi majira ya saa nne asubuhi jijini Mwanza rapper huyo alienda kwa mama yake mkubwa na kumkata sikio.
“Dudu kafanya hivyo, nimejaribu kufuatilia ,duh inasikitisha,lakini sasa ndio hivyo kashafanya, kaenda kwa mama mkubwa kule ,kaenda kamkata sikio jana (juzi). Sababu haijulikani, sababu gani kaenda kufanya kitu kama hicho. Hata kama alikuwa na sababu sidhani kama ni busara kwenda kumkata,kwa madai kuwa mama mkubwa alikuwa anamloga Dudu mambo ambayo hayana hata msingi kwa ujulma,kwasababu hata ukiangalia anamloga kivipi!! Yeye ni mtoto haumwi na hana matatizo yoyote. Mwanae sio mgonjwa ni mzima tu, mimi nikashindwa kuelewa, sasa bibi mkubwa akawa ameleta mtafaruku kwasababu wanae hili suala hawajakubaliana nalo,ikanibidi mimi niende nikazungumza nao pale,tukaenda polisi tukaongea na maaskari, basi tukajua namna ya kumtafuta. Kwahiyo akikamatwa ndio ataeleza alifanya hilo tukio kwa sababu gani, au labda pengine aliagizwa na nani,” alisema.

0 comments:

Post a Comment

Recent Posts