Home
» Enterteinment
» WEUSI WAFANYA REMIX YA GERE KENYA, WAWASHIRIKISHA COLLO NA RABIT, PIA KUFANYA COLLABO NA NAZIZI
WEUSI WAFANYA REMIX YA GERE KENYA, WAWASHIRIKISHA COLLO NA RABIT, PIA KUFANYA COLLABO NA NAZIZI
Rappers wa kampuni ya Weusi Joh Makini, Nikki Wa Pili na
G-Nako wako jijini Nairobi ambako waliperform katika uzinduzi wa video ya Navio
kutoka Uganda Jumanne wiki hii. Wakiwa huko Weusi wamefanikiwa kufanya collabo
na baadhi ya wasanii wakubwa wa kenya.
Joh Makini ameiambia Bongo5 kuwa Kati ya Wasanii ambao
wamefanikiwa kufanya nao collabo wakiwa Kenya ni pamoja na King wa Rap Collo na
Rabit ambao wamehusika katika Remix ya single yao mpya ‘Gere’, na kuongeza kuwa
wanatarajia kufanya Collabo nyingine na rapper wa Necessary Noise, Nazizi.
“Collabo yetu na Nazizi ipo kwenye process nadhani leo ama
kesho jana alikuwa amechoka..” Alisema Joh.
Kazi hizo zimefanyika katika studio ya Love Child ya Wyre pamoja
na Waweshi.
0 comments: