MADEE ALALAMIKA BAADA YA WIMBO WAKE KUONDOLEWA KWENYE KTMA 2014



Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA limeziondoa nyimbo tatu kwenye mchakato wa tuzo za muziki Tanzania, KTMA kwa madai kuwa zinakiuka maadili ya Kitanzania. Nyimbo hizo ni pamoja na ‘Nimevurugwa’ wa Snura, ‘Uzuri wako’ wa Jux na ‘Tema Mate’ wa Madee.







Akizungumza suala hilo leo baada ya kupata taarifa ya kuondolewa wimbo wake kwenye tuzo hizo, Madee amesema hajapendezwa na hatua hiyo.



“Sichukui hatua yoyote ila nawashangaa tu hao viongozi ambao wanahusika na mchakato mzima. Sisi tunaandika nyimbo ambazo vijana wetu wanazipenda,kwahiyo kama wameamua hivyo basi wawe wanatuandikia wao nyimbo,kwasasabu sisi tunawaandikia vijana wenzetu, sasa unakuta hao wanaoendesha mchakato ni wazee hawawezi kuchanganua maneno yetu,ifike time sasa wawe wanatuandikia mashairi,” amesema Madee.


0 comments:

Post a Comment

Recent Posts