LUPITA NYONG’O AUMALIZA MVUTANO WA URAIA WAKE KATI YA MEXICO NA KENYA
Mwigizaji wa Hollywood Lupita Nyong’o ameendelea kuwa kwenye
headlines kutokana na mafanikio ambayo anaendelea kuyapata huko Hollywood,
kiasi ambacho hadi ulizuka mvutano kati ya mashabiki wake wa Kenya na Mexico
ambao wote walikuwa wakidai Lupita ni wa kwao.
Lupita na wazazi wake
|
Hatimaye mshindi huyo wa tuzo za Oscar ameumaliza mvutano
huo kwa kutoa msimamo wake juu ya uraia wake.
“Mimi ni Mmexico na Mkenya kwa wakati mmoja” alisema Lupita.
“Nimekuwa nikiona mvutano juu ya uraia wangu, lakini mimi ni Mkenya na Mmexico
kwa wakati mmoja.” Alizungumza Lupita kwa mujibu wa El Mañana na kusisitiza
tena “So again, I am Mexican-Kenyan and I am fascinated by carne asada tacos.”
Lupita alizaliwa Mexico miaka 31 iliyopita lakini wazazi
wake wote ni Wakenya, na baadae walirudi Kenya ambako alikulia hadi
alipofikisha miaka 16, wazazi walipoamua kumrudisha Lupita Mexico ili
akajifunze Spanish.
Alipoulizwa tuzo alizopata kama zinamilikiwa na Mexico,
alisema “Tuzo ni za kwangu”.
0 comments: