KUHUSIANA NA MIRATHI YA MAREHEMU KANUMBA, BABA YAKE AMEDAI PATACHIMBIKA!!!!

Ni zaidi ya mwaka mmoja umepita toka kufariki kwa mwigizaji staa wa Tanzania Steven Kanumba, ambae aliacha kampuni ya kutengeneza filamu aliyokua akiimiliki pamoja na mali nyingine yakiwemo magari.

Baba mzazi wa Marehemu Mzee Kanumba anaeishi 87.5 Shinyanga amesema ‘kwenye mirathi tumeshirikiana na Mama Kanumba ingawa Jaji kachanganya baada ya kuwekwa watoto ambao sio wangu… mimi na mama Kanumba ni sahihi ila watoto ambao sio wangu tumeandaa Mwanasheria kuwaondoa wasiohusika na tumbo langu vinginevyo na wa tumbo langu waingie kwenye mgao wa mirathi’

‘Watoto walioshirikishwa na sio wangu ni Seth Bosco ambae ni mtoto wa shemeji yangu mdogo wake mama Kanumba, Tina Mshumbuzi, Bella Kajumulo yani haya majina unayaona yako tofauti, hawa wawili nilikuta Mama Kanumba ameshazaa.. kwa hiyo hawawezi kuingia kwenye kurithi ndio maana nafatilia Mahakama itende haki na watoto wangu waingie mule vinginevyo aisee patachimbika’ – Baba Kanumba

Kwenye sentensi ya mwisho Baba Kanumba amesema ‘Kanumba hakua na mke wala mtoto hivyo hawezi kuingia mwingine pale, mirathi ni ya watu wawili mimi na Mama Kanumba tuliemleta duniani Kanumba, sijawasiliana bado na Mama Kanumba…. tutawasiliana Mahakamani’

Baba Kanumba ambae hakuweza kuhudhuria maziko Dar es salaam kutokana na kuumwa, anasema kwenye mazungumzo ya mwisho na Marehemu siku kadhaa kabla ya kufariki, alimwambia kuhusu pesa zaidi ya milioni 50 alizokua nazo benki pamoja na nyumba aliyokua ameianza ujenzi Dar es salaam.

0 comments:

Post a Comment

Recent Posts