SITTA: Tanzania haitambui maamuzi yanayofanywa na wanachama EAC

Tanzania imetoa msimamo juu ya jumuiya ya afrika mashariki na kusisitiza haitatambua maamuzi yoyote yatakayojadiliwa na kuamuliwa na baadhi ya nchi wanachama nje ya utaratibu wa jumuiya.

Akijibu swali la mbunge wa Viti maalum mhe. RUKIA AHMED  nini msimamo wa serikali juu ya mambo yanayohusu jumuiya ya Afrika Mashariki kujadiliwa nakutolewa uamuzi bila ya Tanzania kushiriki.

Waziri wa Afrika Mashariki Mheshimiwa SAMWEL SITTA Amewataka wabunge na watanzania kutambua Tanzania iko makini katika kufuatilia yanayojitokea katika ndani ya nchi wanachama wa jumuiya ya afrika mashariki.

Akijibu swali la Mmbunge wa Same mashariki mhe anne kilango malecela aliyehoji kwa nini Tanzania imekaa kimya katika kuchukua maamuzi, mheshimiwa SITTA amesema serikali haijakaa kimya kuna hatua inazichukua na kusisitiza mamlaka kuu wamekumaliana kutokushiriki katika vikao vyote ambavyo nchi nyingine tayari wanaagenda zao.

0 comments:

Post a Comment

Recent Posts